January makamba aanzisha SMS na wananchi wa Bumbuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

January makamba aanzisha SMS na wananchi wa Bumbuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Feb 1, 2011.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nikitumia maneno yangu nitaonekana mwenye chuki. Haya ni maneno ya January mwenyewe akiongea na viombo vya habari. Hebu niambieni huyu dogo katoa hela wapi??? Mshahara hata bado hajapewa. alikuwa tu mtumishi wa serikali wa kawaida, ila alitumia mgongo wa ikulu kwenye dili nyingi. Wahindi walimpa kiasi cha Millioni 600 kwenye kampeni zake. Dadake wa hapa Vodacom anafanya ufisadi, hawezi kutoa grant kabla ya 30% ambazo zinarudi kwenye mfuko wa January. Kwenye malaria NO MORE alichota zaidi ya $200,000 akishiirikiana na Ruge Mutahaba. hivi hawa ndio viongozi wa Tanzania? Nauliza tu

  MBUNGE wa Bumbuli, Januari Makamba, amezindua huduma ya mawasilino na wakazi wa jimbo lake ambao watakuwa wanatuma ujumbe mfupi katika simu zao na gharama za malipo zinakuwa chini yake.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makamba alisema mawasiliano ya simu ni muhimu katika kuharakisha maendeleo.

  Alisema kwa kuzingatia hilo , wananchi wa Bumbuli lazima wawe miongoni mwa mamilioni ya Watanzania wanaopaswa kuwa na mawasiliano hayo, ili nao wapige hatua za haraka maendeleo.“Nimefanya mazungumzo na kampuni za simu,lengo ni kuleta mawasiliano karibu ili wananchi wangu waweze kunufaika na mpango huo. Nitafanya semina elekezi ya viongozi ili waweze kuwahamasisha wananchi wa Jimbo la Bumbuli kuhusu mpango huo,”alisema Makamba.

  Mbunge huyo wa Bumbuli aliandaa semina ya viongozi wa kata, viti wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kupangiana majukumu ya kutekeleza Ilaani ya CCM.Alisema kwa kipindi kirefu, wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaendeleo na kwamba hadi sasa bado wako nyuma.

  Alisema kwa msingi huo, kuna kila sababu za kubuni mikakati ya kujiletea maendeleo kwa haraka.“Kwa miaka mingi sasa tumekabiliwa na tatizo la kutafuta maendeleo na bado hatujafanikiwa, lakini nadhani wakati umefika wa kutoka kwenye boksi na kufanya kazi kwa bidii ili tupate maendeleo,”alibainisha. Kwa mujibu wa Makamba, wajibu wake kutekeleza ahadi alizotoa kwa wananchi wa jimbo hilo, ambalo kabla ya uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, lilikuwa linawakilishwa bungeni na Wiliam Shellukindo ambaye alishindwa katika kura za maoni ndani ya CCM.

  Mbunge huyo wa sasa, aliwataka wananchi kushirikiana na viongozio wao, ili iwe rahisi kutekeleza mikakati ya kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.
  Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Sophia Mjema, aliwataka viongozi wote walioko madarakani, kutekeleza ahadi zao kwa wakati.Hali kadhalika aliwahimiza watendaji wa vijiji, kuwasomea wananchi mapato na matumizi ya fedha wanazochanga, ili kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

  Alisema kufanya hivyo, kutawafanya wananchi wawe na imani na viongozi hao.
  Wakati huo huo, baadhi ya wananchi walitoa malalamiko yao kwa uongozi wa Jimbo hilo kuwa, baadhi ya watendaji wa kijiji wamekuwa wakiwatoza fedha katika kupata huduma mbalimbali.Huduma hizo ni pamoja na kupigiwa mihuri, kuandikiwa barua na kadhalika.Kuhusu hilo, Mkuu wa Wilaya alionya viongozi wa vijiji kuacha mara moja kuwatoza wananchi gharama za mihuri au kuandikiwa barua

  Chanzo Mwananchi
   
 2. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tanzania tumeibiwa vya kutosha, sasa tuseme basi!!!!
   
 3. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hawa wakina January dawa yao inakuja tu. Nikama vile hawaoni ya Tunisia na Egypt. Hizo hela angeweka atumie uhamishoni (Oman) Uharabuni na familia ya Kikwete. Makamba na kikwete ndio wakwanza kukamata na kuchoma moto siku tunaamua kuchukua nchi yetu, wattoto wao wanafaihidi ufisadi nao hawatapona kamwe
   
 4. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145

  Well said mkuu. Kwakweli kuwa mwananchi kwenye nchi maskini ni mzigo lakini kuwa mwananchi kwenye nchi maskini inayoongozwa na viongozi wenye umaskini wa fikra na tamaa iliyopita kiasi ni mzigo mkubwa zaidi.
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Ndio maana NSSF wameamua kuchukua mali zao zilizo porwa na Mbowe
   
 6. S

  Selemani JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hizi ni chuki tu na ushabiki wa kiitikadi. Huyu jamaa kaamua kuwekeza jimboni kwake na kuleta maendeleo lakini bado mnachonga tu. What more can he do?

  The level of hypocrisy in this place is unbelievable. Au kwa sababu wabunge wenu mliowachagua wako busy kuandamana na kusaka cheap umaarufu instead of bringing about maendeleo?
   
 7. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Mimi sioni chuki hapa. haya ni maneno ya january mwenyewe wakuu. wanachouliza wanajamii ni kwmaba hela kato wapi? Hilo ndo jibu linalohitajika
   
 8. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Januari amepata wapi hela...?????

  Hii ni kashfa kubwa sana... Yeye badala ya kuelekeza nguvu kwenye elimu yeye anafanya jitihada kwenye mawasiliano wanawasiliana nini?
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Haya mambo ya kukurupuka yanazidi kila siku... Anyway soma hapa chini
   
 10. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukirejea makamba na website yake,utajua ni nani anasaka huo u cheap popularity...:twitch:
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Hii nchi ishanyonwa balaa!
   
 12. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mjepu sijakuelewa kabisa hapo Mbowe kaiingiaje??

  Na hao NSSF pia ni wezi pia wakichunguzwa huko watu au viongozi wa juu wamejikusanyia mengi wameshindwa kuendeleza mradi wa NSSF kwa kuwanufaisha wanachama wake

  NSSF wanatakiwa kuboresha na kubuni mikakati ya kukuza miradi yao na sio

   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hujakatazwa kuwa na website yako...
   
 14. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :twitch::coffee:

  inaelekea wewe ndio wale mnaopenda ligi za kitoto,hata wewe hujakatazwa...kaanzishe!
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,381
  Likes Received: 19,656
  Trophy Points: 280
  bora aibe halafu awasaidie watanzania kuliko vijisenti angezipeleka uswis
   
 16. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Hukuna wizi ni wizi na pia huyu january makamba dada yake yupo voda na rostam ni mmoja wa wamiliki wa wa voda tulitafalkari hili
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ulimbukeni bado ni tatizo kubwa sana
   
 18. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yeah,i was right wewe ndio waleeeeee.....mliocheza ligi za mchangani hata humu mtandaoni mnaona sifa saana kuanzisha ligi zisizo na kichwa wala miguu CHUKUA TIME HUKO,kati yangu mie na wewe limbukeni anajulikana wazi ni nani......and this is my last post kukujibu,andika unalojisikia kuandika ila sitakujibu!mxysssssssss!:twitch:
   
 19. mkokoteni

  mkokoteni Member

  #19
  Feb 1, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Pale nchi inapokuwa na viongozi wafadhili staili yao ndo kama hiyo. kutumia umaskini wa wananchi kujijengea umaarufu na uhalali. Badala ya kufungua fursa za kiuchumi , ilikukuza kipato cha wananchi, kiongozi anatoa sms za bure. Kwahiyo habari hapo haijaonyesha sms za mtandao upi au mitandao yote. hauhitaji huduma ya sheikh ya utabiri kujua kuwa ni mtandao gani hou kama sio vodacom... kila mtu anajua hilo.

  Mbunge mmoja wa singida alisema ubunge wake 2005 - 2010 alitumia pesa zake binafsi 2.5 billion shillings kwenye maendeleo ya jimbo. hawa ni viongozi wafadhili. unahita wanazuoni (Reseachers ) waje wafanye utafiti wahali tabaka jipya lilichipuka ghafla nchi tanzania. tafakali
   
 20. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu a fruit does not fall far from the tree it came from. Mimi nilisha-connect dots siku nyingi sana.
   
Loading...