TANZIA Janka wa LWP afariki dunia

TANZIA Janka wa LWP afariki dunia

NGAYANIMO

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
36
Reaction score
55
Tasnia ya muziki wa bongo fleva, hususan muziki wa Rap wa zamani kutoka kwenye viunga vya wilaya ya Temeke, imepata pigo kufuatia kifo cha aliyekuwa mwanzilishi wa kundi la Rap la LWP (Majitu), Salum Ngwele maarufu kama Janka Rhino.

Janka ambaye pia alikuwa kiongozi wa kundi hilo la Rap lililojizolea umaarufu mkubwa kutokana na staili yao ya kipekee ya kurap, amefariki dunia mapema leo na anatarajiwa kuzikwa kesho saa 7 mchana kwenye makaburi ya Temeke Wailes.

Akiwa na waasisi wengine wa kundi hilo kama Haji Kibombozi (QG), Hamis Kibavu (Dj Flex), Issa Iddi (Slaughter) na wengineo, atakumbukwa kwa mengi aliyoyafanya katika kuhakikisha kundi hilo linasonga mbele na kuwa moja ya makundi maarufu ya Rap kutoka Temeke.

Wimbo wao maarufu wa "Jitu Kali" ni moja kati ya track ambazo marehemu alishiriki kikamilifu katika uandishi, na kurap verse ya mwisho (ambayo kipande chake kinasikika kwenye post hii) na kuimba kiitikio cha wimbo huu uliolitangaza vyema kundi la LWP.

Msiba upo nyumbani kwao Temeke Mwembe Yanga, na taarifa hizi nimejulishwa kwa njia ya simu na marapa wawili wa LWP, Hamisi Kibavu (Dj Flex), na Issa Iddi (Sloter). Mungu alilaze roho ya marehemu Janka Rhino mahali pema peponi, Amen.

RIP Soldier

Tutaonana Baadae

Screenshot_20260227_083502_Lite.jpg
 
Wanaokwenda Jela
Mke wa Mtu
Jitu Kali - Jitu Jambazi

Poleni ndugu ,jamaa na marafiki ,poleni L.W.P -Living With Purposes ,Pole "SLOTA".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom