Mungu Mweusi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 1,474
- 1,079
Habari wanajamii, Poleni na hongereni kwa majukumu ya ujenzi wa taifa.
Tukiwa kama familia moja nimependa kuuza wazo hili la kijamii. Jamii yetu ina matatizo na changamoto nyingi ambazo kwa umoja wetu hatuna budi kushirikiana na serikali na taasisi binafsi katika kutatua matatizo haya.
Narudi kwenye Agenda; tukiwa tunajiandaa na Sikukuu ya Maulid, Krismas na Mwaka Mpya watu wengi kwenye jamii tumejipanga kusherekea kwa namna tofauti.
Kwa kuvaa mavazi mapya, kula vyakula tofauti, kunywa, kucheza, na anasa nyingine tofauti lakini kuna makundi ya watu ambao hawana uwezo wa kula, kuvaa, kucheza, wala kushiriki chochote katika MWAKA mzima. wamekosa furaha, wametengwa, wagonjwa, na shida nyingine tofauti.
Hivyo nimependa kuwashirikisha hili ili tupange namna ya pekee kusaidia makundi hayo. Hivyo napenda kwa umoja wetu kupanga namna pekee ya kwenda Kusaidia WAZEE wanaoishi KAMBI ya WAZEE BUKUMBI, MISUNGWI-MWANZA ili nao waweze kufurahia mwisho wa MWAKA 2015.
Hata kwa kupata chakula na vinywaji. Nawasilisha Hoja