Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Leo katika ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl, nikiwa mmoja wa watetezi/wanaharakati wa Haki za binadamu nimepata fursa ya kuhudhuria maadhimisho tajwa.
Pia kuna wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi, Kuna mabalozi mbalimbali pamoja na wanaharakati wa haki za Binadamu Tanzania na nchi nyingine za Maziwa Makuu.
Pia nimefurahia uwepo wa Banda La JAMII MEDIA (JamiiForums) katika moja ya mabanda ya Maonyesho.
Mambo mengi yamezungumziwa kuhusu unyongwaji wa haki za binadamu. Jinsi vyombo vya dola kama polisi jinsi vinavyotumia nguvu walizopewa kunyanyasa Raia bila sababu za msingi.
Pia katika Documentary wamezungumzia jinsi kiongozi wa waliohitimu mafunzo ya JKT Ndugu George alivyotekwa, kuteswa, kuminywa haki zake kama binadamu na kutupwa kwenye pori kisa alikuwa mstari wa mbele kudai haki zake za msingi kupatiwa ajira,
Soma;
Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu wajitosa sakata la kuteswa kwa mwenyekiti wa JKT.
Kiongozi wa vijana wa JKT, George Mgoba apatikana Msitu wa Tumbi