Jamhuri yashindwa kesi ya dawa za kulevya

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303


Mkazi wa Same mkoani Kilimanjaro, Aizak Mgavao aliyekamatwa kwa kosa la usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi ameachiliwa huru leo Jumatatu na Mahakama Kuu ya Moshi baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kutoa vielelezo kamilifu.

Akitoa taarifa hiyo Jaji Mfawidhi Kanda ya Moshi, Aishael Sumari amesema mtuhumiwa hana kesi ya kujibu kutokana na mkanganyiko wa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri hivyo ameachiliwa huru.

Aizak alikamatwa mnamo Aprili 11 mwaka 2015 katika kituo kikuu cha polisi Moshi akiwa na mirungi kilo 111 yenye thamani ya Sh 5.5 milioni.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwahiyo hana kesi ya kujibu pamoja na vithibiti vyote hivyo? Sitaki kuamini , kama ni kweli basi hakuna haja ya kuwakata
 
mirungi taratibu wataipa uhuru kuwa kitu cha kawaida.
 
Reactions: SDG
Ni agharabu sana Jamhuri kushinda kesi
 
Mkuu
Babati
Jamhuri Inapaswa Kulipa Usumbufu
Hii Ilipaswa Mahakamani Pale Jaji Aseme Wazi
 
Mkazi wa Same mkoani Kilimanjaro, Aizak Mgavao aliyekamatwa kwa kosa la usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi ameachiliwa huru leo Jumatatu na Mahakama Kuu ya Moshi baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kutoa vielelezo kamilifu.

Akitoa taarifa hiyo Jaji Mfawidhi Kanda ya Moshi, Aishael Sumari amesema mtuhumiwa hana kesi ya kujibu kutokana na mkanganyiko wa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri hivyo ameachiliwa huru.

Aizak alikamatwa mnamo Aprili 11 mwaka 2015 katika kituo kikuu cha polisi Moshi akiwa na mirungi kilo 111 yenye thamani ya Sh 5.5 milioni.

*Vita ya dawa za kulevya haijawahi kumwacha mtu salama* (In DAB voice)
Source: mwananchi
 
nataka kujua kwanini mirungi na bangi ziko kundi za dawa za kulevya kwa mantiki ipi??
 
Duh huo uamuzi wa hakimu kama ndio uko kama ulivyoandikwa kwenye gazeti basi ni bora tusiwe na mahakimu
 
Duh huo uamuzi wa hakimu kama ndio uko kama ulivyoandikwa kwenye gazeti basi ni bora tusiwe na mahakimu
Pole mkuu, unaonekana umeandika kwa uchungu sana. Lakini ndo hivyo tena, taaluma zisipoingiliwa na nguvu kutoka juu, haki huwa zinatendeka hata kama ni dhidi ya serikali. Hongera ndugu wa mirungi, ila usirudie kama ni kweli ulionja kidogo
 
Kwa DPP kuna wanasheria viazi sana.kesi zote za madawa ya kulevya siku zikifika court of appeal watu wote wanamwagika..ni ujinga mtupu kwenyw hizo kesi..unasema mtu kakamatwa na madawa airport katoka nayo brazil halafu huna passport kama ushahidi! Si wendawazimu huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…