Mwanagenzi
JF-Expert Member
- Sep 11, 2006
- 724
- 249
Kwa majuma kadhaa gazeti la Jamhuri, Wanaanzia Wengine Wanapoishia, limekuwa likiripoti habari juu ya tuhuma za Kampuni ya Bia Tanzania, TBL, kufanya udanganyifu kwa lengo la kukwepa kodi. Sijabahatika kupata nakala hata moja ya gazeti hilo, na niombe kwa mwenye uwezo, hususan Manyerere Jackton, aniwekee (nijisemee mwenyewe) au aweke humu jamvini ripoti hizo za kiuchunguzi kama zilivyochapishwa ili mimi mwenye nia ya kuelewa zaidi na kufuatilia juu ya suala hilo niweze kujielimisha.
Naomba kuwasilisha, kwa heshima na taadhima.
Naomba kuwasilisha, kwa heshima na taadhima.