James Mbatia: Polisi Tanzania ndio Magaidi namba moja

seedfarm

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
260
2,654
Akizungumza na waandishi wa habari James Mbatia amesema Freeman Mbowe sio gaidi bali magaidi ni polisi wanaochochea chuki kwa wananchi

James Mbatia amesisitiza Kitendo cha Polisi kuingilia na kuvamia mikutano ya ndani ya siasa ni vitendo vya kigaidi kwani wamewasababishia chama hasara Kubwa sana ya kuaanda mkutano

James Mbatia amesisitiza IGP Simon Sirro na kamanda wa kanda maalum Dar es Salaam hawapokei simu bali wanatumia tozo za miamala vibaya kwa kuvunja katiba na sheria za nchi

Mbatia anasisitiza kuwa Jeshi la polisi linatumika Kueneza Chuki na kukandamiza Raia, Hivyo Jeshi la polisi ndio magaidi namba moja Tanzania

James Mbatia anasema Polisi wanatumika Kueneza Chuki na ugaidi nchini huku wakitumia magari na vitendea kazi vya kodi ya wananchi
 
Nilisikiliza leo tena ya clouds kwamba kuna mtu alichambwa mpaka akazimia sasa tufanye kuchamba
 
Tatizo wana siasa wa Tanzania mnachukuliaga tatizo ni hadi likupate wewe ndio unaona ni tatizo ila likiwapata wananchi wakati wewe halikugusi huwa wala hamjisumbui au likimpata mwanasiasa mwenzio mnaonaga poa tu. Laiti mngekuwa mnajitambua kazi ya kupambana na ccm ingekuwa rahisi sana, ila nyie wote mnahangaikia matumbo yenu.

Wewe Mbatia wakati Chadema wanazuiwa mikutano yao ya ndani mwaka jana wewe si ndio ulikwenda Ikulu kunywa juice wewe na kuwadhihaki Chadema? Ukalipiwa na nauli na per diem kwenda mikoani wewe kuwananga upinzani wenzio? Sasa deal limeisha uchaguzi umepita umejigundua kuwa wewe ni condom tu umeshatumika umetupwa, unalia nini sasa, furahia maisha yako humo jalalani ulipo.

Mnatuchosha sana wananchi na kama hamjui mnasababisha watu wengi ambao hawaipendi ccm wanakuwa neutral tu, wanaona ujinga tu kuwasapoti hata nyie wapinzani.

Unganeni acheni ujinga, jitambueni.
 
Duuuh! Kasema Polisi ni magaidiii? Na tunawalipa mshahara.
Jamaniee tuhamieni Burundi tuache ubishi hiinchi siyetuu hatuhitajiki hapa.
 
Mbatia used to be a very serious opposition leader until when he was bought by CCM by being made M Pi
 
Akizungumza na waandishi wa habari James Mbatia amesema Freeman Mbowe sio gaidi bali magaidi ni polisi wanaochochea chuki kwa wananchi

James Mbatia amesisitiza Kitendo cha Polisi kuingilia na kuvamia mikutano ya ndani ya siasa ni vitendo vya kigaidi kwani wamewasababishia chama hasara Kubwa sana ya kuaanda mkutano

James Mbatia amesisitiza IGP Simon Sirro na kamanda wa kanda maalum Dar es Salaam hawapokei simu bali wanatumia tozo za miamala vibaya kwa kuvunja katiba na sheria za nchi

Mbatia anasisitiza kuwa Jeshi la polisi linatumika Kueneza Chuki na kukandamiza Raia, Hivyo Jeshi la polisi ndio magaidi namba moja Tanzania

James Mbatia anasema Polisi wanatumika Kueneza Chuki na ugaidi nchini huku wakitumia magari na vitendea kazi vya kodi ya wananchi
Absolutely true
 
Back
Top Bottom