Jamani watu wa kiswahili nisaidieni,hii mbona ngumu?

Naomba nijaribu hapo VIYEYUSHO ni KONSONANTI ambazo zinazotamkwa kama IRABU. katika kiswahili kuna aina mbili za VIYEYUSHO navyo ni: "W" na "Y" vipashio hivi viwili katika kutamka huweza kutamkwa kama IRABU. Kipashio "W" hutamka kama IRABU "U" Mfano: "Wanacheza" inatamkwa "Uanacheza" utakubaliana na mimi kama utaweza kutamka vema neno hilo, lakini pia kipashio "Y" kinatamkwa kama IRABU "i" mfano: "Yale" inatamka "iale"Sababu hiyo ndio inayofanya vipashio hivi kuitwa VIYEYUSHO. Vilevile katika lugha ya kiingereza vinaitwa SEMI-VOWEL ambavyo ni "W" na "J" Hii ni kwa mujibu wa uwezo wangu. Sijui kama nimekuelewesha kidogo au nimekuchanganya
 
kwahyo Y ni kiyeyusho na pia ni kipashio? Kipashio nacho ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…