The golden
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 1,381
- 2,553
Kadri siku zinavyokwenda nazidi kujifunza, moyo wangu unapondeka, unyenyekevu unatawala.
Kwanza kabisa, nimepoteza watu wengi sana wa maana katika maisha yangu, watu niliowapenda na kuwategemea, kwa kiasi fulani walinijengea kiburi.
Nimewaona watu wenye mamlaka na nguvu kubwa wakitoweka ghafla kama upepo, hili nalo limepunguza majivuno yangu. Kuna watu walikuwa na sauti ya kutisha, wangeweza kufanya chochote, kusema chochote, au kumfanya mtu mwingine chochote hawa nao hawapo, na wengine wako gerezani.
Siku zinaenda kasi sana, jana siyo sawa na leo. Leo unaweza kucheka kesho ukaamuka unalia.
Mimi nimechagua haki, upendo, na unyenyekevu. Dunia wala Tanzania si mali yetu, dunia tuliikuta na Tanzania tuliikuta, vyote tutaviacha.