Jamani Trafic mtatuua

sir mweli

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2017
Posts
495
Reaction score
575
Hii ni wiki ya pili kila nikilala naota Nmekamatwa na Trafic. Leo asubuhi nimeamka naenda kuoga nakutana na jirani yangu nae katoka kuoga kajifunga taulo jeupe na kichwani kavaa mfuko mweusi kuzuia maji... Nkashtuka kidogo nirudi ndani speed maana nmeona kama Trafic vile.
Jamaani kama ni njaa tunayo wote.. Si nyie tuu... Mtuonee huruma na sie.
 
Chini hakuvaa Viatu vyeusi? Kama una kapicha weka tuone
 
Nchi imepinda wacha wainyooshe cha ajabu sisi walala hoi ndo tunanyooshwa
 
 
Cha ajabu hata jero hawaachi
mkuu kama wangekuwa wanachukuwa jero si afadhali ila saiv dau kubwa

Yaan hawa jamaa utasema kama hawakai mtaani na bora wajengewe nyumba zao wahame mitaa yetu maana hatutaki hata kuwaona
 
Mara nyingi mhalifu akiona polisi anashtuka sana.....anaweza hata kutimua mbio!
 
Juzi kati nipo na jamaangu kanunua volkwagen yake brandnew.. Mara trafic huyu hapa.. Kakagua kila kitu hajapata kosa... Haya washa indicator jamaa akawasha.. Trafki kadai eti indicator zinategeana.. Haziwak kwa wakati mmoja..akaandika kosa hilo.. Haya fungua buti ya nyuma... Kakuta engine... Anadai anataka documents za hiyo engine.. Mmebeba engine kwenye buti mnapeleka wap... Kosa jingine hilo akaandika... Duuh Trafk mnatusomesha namba kwa lazima.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…