Sidhani kama huyo mkaka hata anajua maana ya kupenda. Ningemshauri huyo mtoto wa anti yako atulie tu maana Mungu amemuepusha na balaa kubwa sana, huyo mwanaume sio mwaminifu na sidhani hata kama na huyo mdogo wako watadumu cos wazuri wanazaliwa kila siku.
aache hasira zake. wewe tulia.... kama jamaa yupo serious na dogo waache waendelee na yao na huyo mtoto wa anti atapata mwingine. mambo ya mapenzi hayanaga usuluhishi na wala hakuna kuyawaziawazia.... wewe tulia. muda tu ndo utasuluhisha maana naye huyo mtoto wa anti atapata mwingine na kusahau yaliyopita.
Asante kwa ushauri. ila hofu ipo kwa mama maana hajajua kwa nini mtoto wa anti kaondoka nyumbani
Ndani ya moyo wako una hatia?namaanisha unahisi umechangia kwa vyovyote vile hayo kutokea?kama moyo wako uko u msafi na unaamini hujapelekea hayo kutokea basi Mpe muda huyo mtoto wa shangazi yako ataelewa kila kitu!Wasiwasi weka kwa mdogo wako na kama unaweza mshauri awe makini na wakaangalie afya zao yeye na huyo shemeji yako!wakikataa mshauri acheze salama!
Jaribu kumwambia ukweli kuwa wewe na familia yako have nothing to do with that,pia mwambie suala la wale kuwa wewe hausiki na kilichotokea,kama ni ujinga ni wa mwanaume kutokuwa mwaminifu,tena ashukuru huyo jamaa amejionesha yeye ni nani mapema,ayakubali matokeo,kama hataki kukusikiliza mwache muda ukipita atajirudi mwenyewe usimlazimishe akuelewe!
asante ndugu yangu
Dah, inaonekana hao ndugu zako wanajua kupenda! Mtoto wa shangazi kazimika kichizi hata kabla ya kumuona jamaa, na mdogo wako pamoja na kujua hivo kaingia kichwakichwa bila kujali ndugu yake atajisikiaje! Tamaa?! Huyo ndugu yako ataponywa na mda, kadiri siku zinavyopita atazoea na atamshukuru Mungu kwa kumuepusha na mtu mwenye tamaa na asiyejali.