Nimekuwa naishi na mdogo wa mke wangu. Yaani shemeji yangu amekuwa akiishi kwangu yeye na mtoto wake kwa zaidi ya miaka miwili. Huyu shemeji yangu alikuwa ameolewa ndowa ilivyo mshinda akahamia kwa dada yake yeye na mwanaye.
Sasa imefika mahali nikawa najiuliza nitaendelea kutuza familia ya mtu mwingine bila faida yoyote mpaka lini? Sasa siku moja nikajitia uchizi nikasema kwa vile nahudumia kila kitu basi angalau nimuombe huyu shemeji mapenzi ili nipoze machungu ya kulea mama na mtoto wa mtu mwigine.
Basi nilivyo tu jaribu shemeji akakasirika akaenda kumwambia dada yake . Sasa dada yake anasiku mbili ni kulia tu haongei na mimi hata kidogo . Watoto wnauliza baba umemfanya nini mama mbona analia sana, nashindwa cha kusema. Na mimi nimeamuwa nikae kimya siongei na shemeji wala mke wangu .
Naongea tu na watoto. Kila nikimwambia tuongee anakaa kimya na kuendelea kulia. Sasa ndio nimekuja kuomba ushauri kwenu. Najuwa humu kuna watu wengi huwenda kuna mtu kapitia changa mto kama yangu . Karibuni wote kwa ushauri.