Jamani nimebahatika kupata mil 30, nianzishe mradi gani utakaonitoa mazima?

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,408
Wadau kuna kampuni imenilipa fidia ya sh mil 30. Kulitokea nini na ilikuwaje mpk nikalipwa fidia hii? Nisingependa kuiongelea.

Ombi langu kwenu ni kwamba naombeni ushauri na uzoefu wenu wa kuiendeleza fedha hii ili nisije rudi tena kwenye umaskini wa kukosa milo 2 kwa siku.

Naomba kuwasilisha.

ANGALIZO: Tusileke mizaha na utani tafadhali.
 
Una interest na kufanya nini au una interest na kitu gani? Kuna watu wana interest say ya kulima au kufuga au kufanya biashara ile ya kununua vitu na kuuza aidha vya ndani au kutoka nje ya nchi. Wewe binafsi umekuwa unatamani kufanya nini? Yaani ni kitu gani ulichokuwa unatamani hapo ulipokuwa huna pesa, yaani ulikuwa unasema, siku nikipata pesa nitafanya hiki na hiki au hiki na kile. Kama ndivyo, basi sasa umezipata, kifanye. Ukisha amua ni nini unataka kufanya basi leta wazo lako humu JF usaidiwe kwa mawazo na utekelezaji, if possible!
 
Ngoja waje lakini hakikisha unawekeza mil5 au 10 tu katka hiyo biashara nyingine hifadhi huku ukiusoma mchezo vizuri. Baadae ndio uwe unaongeza mtaji kidogo kidogo.
 
Haoana mkuu. Dadavua kidogo
Hebu kwanza muulize Waziri Jaffo! Any way hii ni njia ya kutumia "nguvu kazi" iliyo karibu nawe, yaani tafuta mafundi wachache wazuri, wawe na vibarua wao wazuri na UFANYE SUPERVISION WEWE MWENYEWE hasa kwenye UNUNUZI WA VIFAA. Kwani hapo ndio tunapo umiziwa zaidi na mafundi. Nunua vifaa mwenyewe. Ule uofisa wako wa 2.4m. weka pembeni na matokeo utayaona.
 
Asante kwa ushauri na maelekezo
 
Mil. 30 haifai hata kujenga banda la kuku
Nilikuwa natamani sana kujenga nyumba za kupangisha. Halafu kisha nakopa benki kwa dhamana ya nyumba hizo hizo naenda kujenga sehemu nyingine. Basi inakuwa ndiyo mwendo wa kukopa na kujenga

Siyakukothamela Sonini na nini
 
Back
Top Bottom