Kazi ya mbunge ni kugawa pesa? kazi ya ubunge ni kuzuia Ukimwi? Kazi ya mbunge kuinua uchumi?
Mimi namtafuta mbunge wangu arumeru mashariki:Jeremia Solomon Sumari - sisiem
Sishangazwi na maswali kwakuwa yanaonesha uwezo wako wa kufikiri kama wa kuku
hahahaaaaaaa yuko ka hotel men,,leo alikua kanisani anatafuta siresireWadau nimekuwa nikimtafuta Mbunge wangu wa jimbo la Rorya ndugu LAMECK AIRO kwa muda mrefu, je kuna mtu kamwona? Katika kikao cha Bunge kilichopita nilimtafuta sana Bungeni lkn sikufanikiwa kumwona. Sijui ana mpango gani na wananchi wake ambao wana shida nyingi sana lkn yeye yupo kimya tu; hivi anajua kwamba Ukimwi unawamaliza wananchi wake? na hali mbaya ya uchumi je? Lameck hata kuchangia kwa njia ya maandishi Bungeni imekuwa tatizo? Je ni nani sasa anayewasemea wananchi wake?
Hivi huyu bado ni mbunge? Naona kanywea baada ya kuukosa unaibu waziri.
Hadi akajenga four star hotel LAKAIRO kule uswahilini kirumba na wewe jitahidi uuze dagaa utatajirika
Bado ni "mbunge mteule" maana hata kuapishwa bado. Yupo hoi kitandani zaidi ya mwaka sasa. Tatizo ni kansa ya ubongo. Inaonekana mtoa roho anamzungukia tu!
teh teh teh!
Pole sana ndugu yangu kwa kutomwona mbunge wako kwa muda mrefu hadi umeamua kujitoa humu inawezekana kura yako ulimuuzia,
Mimi mwenzako namshukuru Mungu kwa kuwa karibia kila siku namwona Mbunge wangu Mh Mchungaji Peter Msigwa akiwa anatoa mawazo, hata kwenye Mwananchi ya leo naye mchango wake umetolewa,
Labda kwa kukusaidia wew pamoja na wazalendo wenzako wa jimboni kwenu niwape nukuu moja isemayo,' Bad Leaders are elected by good Citizens who do not Vote'; George Jean Nathani . Kwa hiyo muda wa kuachana na huyo mbunge umewadia.
Poleni sana kwa kupoteza kura zenu.
mama yangu! Ina maana bado tu wananchi wakamchagua? Mh!