Jamani nahitaji mume mwenye mapenzi ya dhati.

Kila jema bi dada.
Kila mtu anamtu wake hapa duniani.
 
NATA niliposema haijalishi ameajiriwa au amejiajiri nilikua namaanisha kati ya mawili awe ameajiriwa au amejiajiri mwenyewe lakini si mkaa nyumbani na ndio maana nikasema awe anapenda kufanya kazi. mwanaume asie fanya mi wa nini. mi mwenyewe nafanya kazi ye akae nyumbani kasema nani sio kwa maisha ya siku hizi kwa hapo wataniswamehe.
 
NATA hujamwelewa huyo mkuu.. Yaani hachagui kazi ya mchumba wake mtarajiwa. Akiwa na duka sawa,ofisi fulani ya uhandisi au sheria ya kujiegemea,sawa...au awe ameajiriwa kwa wazungu,wahindi,wabongo,au serikalini,nayo pia hajali.
Mradi MPENDA KAZI...

Mh maana vijana wa siku hizi wanapenda mteremko sana!
 
Mwenye upendo wa dhati atakutafuta mwenyewe. Yeyote atakayekuja kutokana na post yako anakuja kwa sababu ni mteremko ila atajifanya anakupenda kwa dhati. Subiri.
 
nina wasiwasi na umbo na sura yako.....miaka 33 hujawahi kuwa na mchumba halafu unataka mtu wa kukuoa faster? ngoja waje wenyewe....
 
Duh,uko tayari kwa Mathna?
 
Awe na umri wa 37-45, anafanya kazi haijalishi ameajiriwa au amejiajiri na awe mpenda kazi, muislam na anaipenda dini. awe na upendo wa bila kuangalia sura wala umbo la mtu.awe tayari kuoa si urafiki.

Ngoja, kuna rafiki yangu yeye ni mwislam......ngoja nimpelekee habari hizi njema. Kwani inajalisha anakunywa au hanywi maana huyu yeye ni chapombe, ila amejiajiri na ana pesa.
 
hii biashara itafanyika kweli,
mbona dada unakuwa mkali as if unalazimisha watu wakuoe!!!!!!
au ww ni msoja? 'manake u sound like'
 
Awe na umri wa 37-45, anafanya kazi haijalishi ameajiriwa au amejiajiri na awe mpenda kazi, muislam na anaipenda dini. awe na upendo wa bila kuangalia sura wala umbo la mtu.awe tayari kuoa si urafiki.

Ngumu hiyo...
 
Nenda katangaze msikitini. Hapa wamijaa matapeli watupu.
 
Awe na umri wa 37-45, anafanya kazi haijalishi ameajiriwa au amejiajiri na awe mpenda kazi, muislam na anaipenda dini. awe na upendo wa bila kuangalia sura wala umbo la mtu.awe tayari kuoa si urafiki.
Mimi sifa zote ninazo ila nimetishika na kipengele hicho hapo kwenye bold. Vipi dada mbona hujiamini, au una sura na umbo kama la "tyson"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…