yesu wangu na maria.....
wewe mtoto wewe .... iyo ni alert tu mungu amekupa kwamba hayo mapenzi uliyoyaparamia kwa pupa ipo siku yatakutokea puani .... tena inabidi ukapime tena maana si ulishangonoka na alex bila condomu?
mimi nakushauri umrudie mungu .....
achana na zinaa na tamaa za dunia hii....
tulia kama mimi ...
soma kwa sasa ,mapenzi yapo nenda taratibu dunia hii....
zamani nilizoea kuona Ukimwi wanapata watu wazimaa na familia zao..lets say miaka 50 na kuendelea.siku izi mambo yamekua tofaut kabisa maskini...kijana kam ahuyo hata bado hajagraduate ameathirika......what a loss to this poor nation and his family!!...am crying ooh Lord!
kwa upande mwingine usimuache gafla ataezakufa....nenda nae tu taratibu maadam alipenda kujua afya yake kupitia wewe..usimuhukumu...ungeweza kuwa umeupata pia..kuwa mtu wake wa karibu maadam ushaiju ahali yake ni rahisi kujicontrol.
NAITWA happy nipo ktk wakati mgumu sana.yote niliyoyafanya leo najutia.wakati nipo secondari.nilikuwa ktk mahusiano na mkaka mmoja kwa jina Alex,kiukweli tulipenda sana ila Alex alikuwa for5 mm for6,kpnd chote icho Alex alikuwa msaada mkubwa kwangu kipesa,kimasomo,hata maradhi,ila mimi baada ya kumaliza for6 majibu yalitoka vizuri baada ya hap...o nikaingia chuo MLIMANI.Nilisoma kwa juhudi zote ila baada ya mwaka mmoja pale chuo nilitokea kumpenda kaka mmoja kwa jina Victa.na mpaka muda huu nipo ktk mahusiano nae.
wiki iliyopita nimeenda kwakina Alex nimemwambia mm na yeye basi Alex amelia sana,ila leo hasubui kanitumia msg.kaniambia sawa happy nimekuelewa kila la kheri.nikamjibu sawa nawe pia.kwa kweli mapenz ya victa yalikuwa matamu sana Juz nilienda mlimani city na victa ila gafla nikakutana na Alex,wala sikuogopa nikamsalimia Alex mambo?then nikamtambulisha kwa victa,alex huyu mpenz wangu anaitwa Victa.alex akanijibu ok poa.baada ya hapo tukaondoka ila kwa sasa kuna tatizo kati yangu na Victa.Victa anapenda sex ya bila kutumia condom,nimemshauri tukapime kwanza jana tumeenda kupima.ila majibu sio mazuri kwan Victa ni mwathirika wa ukimwi.ila mimi niko safi.JAMAN Nataka kurud kwa Alex kwan siwez kuishi na Victa.JE MNADHAN ALEX atakubali kuwa na mimi tena????
Wasichana wengi wanapovuka tabaka moja kwenda jingine mara nyingi hudharau wale waliowaacha nyuma au chini. Mathalani, akipata kazi na mpenzi wake akawa bado ni mtu wa mtaani, ni rahisi huyo wa mtaani kutoswa.
Hapa tumeona mfano hai wa Happy kumwacha Alex vile tu kafanikiwa kufika chuo kikuu na huko kakutana na Victor,so far kijana ambaye kielimu kamzidi Alex.
Dada Happy, inampasa asubiri baada ya muda fulani upite halafu apime tena mara mbili au zaidi ili kwa uhakika kabisa athibitishe kuwa yu mzima.
Pili, kwa heshima ya wanaume wote tafadhali Happy muache Alex aendelee na maisha yake maana awali si kwamba ulitupa tu jongoo, bali ulitupa pia na mti wake.
Mwenyewe kwa matamshi yako hapo juu umekiri kuwa "mwaka mmoja uliopita ulipofika chuoni ulitokea kumpenda kijana mmoja kwa jina Victor"...hivyo sidhani kama kweli Alex ni aina ya mwanume ambaye kwako unaona ndiye akufahaye pamoja na mambo yote mlofanya mkiwa A-Level.
"Majuto ni mjukuu"
Mtumeeeeeeee! yani umeshapona hapo bado hata kukaukamshukuru mungu kakuvua hayo ndio kwanza unataka ushauri wakurejeana na awali? ebu tuliza kwanza ufikiri japo kidogo....