Habari zenu jamani, kuna dada mmoja nilimpenda sana tukiwa form 4, nilivyojaribu kumuambia akaniambia nisubirie tumalize shule, Na mimi nikamuelewa kwa sababu nilikuwa na malengo yangu, nikampotezea.
Tulivyomaliza tukakaa kama miezi 2 then nikamtafuta ili nimkumbushie, cha ajabu alinikubalia hadi sasa hivi ni demu wangu na tunapendana sana, na malengo ni tuje tuoane. Mimi nipo form six, na anasubiria nimalize ili tuendelee na mapenz yetu.
Lakini tatizo kubwa hapa ni UMRI, tunalingana. Je, ni vizuri kuoa mke unaelingana nae au anaekuzidi umri? Naamini nipo ndani ya GREAT THINKS so nategemea kupata mawazo yenye busara.
Nashukuru sana!