Pole sana mwambie awe anapakaa sehemu yenye kidonda Asali safi mbichi ya nyuki kila siku asubuhi na wakati anapokwenda kulala mwambie ajaribu kwa muda wa siku 7 kisha uje hapa utupe feedback . Kidonda chake kiko kama hivi? angalia picha hapo chini....... Samahani kwa watu wasiopenda picha hili ni Jukwaa la JF Doctor atakaye kasirika shauri yake.Naomba kama kuna mtaalamu humu jukwaani asaidie tafadhali!
Kuna tatizo limemtokea ndugu yangu toka mwaka 2005 ikiwa ni kauvimbe mfano wa jipu karibu kabisa na
sehemu ya haja kubwa dr akapasua ila hakikupona tena ila mwaka 2008 hospital nyingine wakagundua ni ni perianol fistula wakamfanyia operation pakapona na kukauka ila mwaka jana hali ikabadilika tena uvimbe na maumivu makali wakagundua ni jipu ile hospital waliomfanyia operation 2008 wakafanya tena operation kwa gharama kubwa. Amepata nafuu ila kuna wakati kunakuwa na kauvimbe kanapasuka (after one to two weeks) wakati wa kujisaidia anaona damu nzito then panakauka kauvimbe kanarudi tena baada ya siku kadhaa?
Ndugu yangu ameanza kukata tamaa, jamani mwanye tiba mbadala au mawazo chanya please saidia tafadhali!
uzito wake na urefu wake tafadhali, alishafanya vipimo?
Fuata maelezo hayo hapo juu niliyoeleza ila upate Asali Safi mbichi ambayo haijachaka chuliwa ajipake atapona inshallah. Na Mgonjwa aende kupima Ugonjwa wa kisukari ili kuhakikisha hana huo ugonjwa wa kisukari. Kama anao huo ugonjwa wa kisukari kidonda kinakuwa tabu kupona.MziziMkavu baada ya operation ndo kilikuwa hivyo ila kikapona ila issue inayosumbua ni hako kauvimbe kanakotokea na maumivu kisha kanapasuka after a week kanarudia tena!
Vipimo amefanya sana na cost zina kuwa kubwa siku hadi siku - Uzito wake ni 65 kg na urefu ni cm 167