pole kwa tatizo lako lilianza ukiwa na umri gani?..... Mimi chuo nimesoma course moja na mtu mwenye shida ya masikio na nilikuwa nae karibu sana tuliishi wote kuanzia mwaka wa 2 mwishoni na watatu......
Unaweza kufanya vizuri kuliko hata wanaosikia kwamaana wanaosikia wengi hawawi attentive na wanajiamini ila wewe ukawa na hiyo advantage.....inabidi uweke wazi shida yako kwa watu wa muhimu kama lecturers, rafiki wawili watatu wa karibu ili ikitangazwa test na sehem za kusoma uwe unaambiwa......
mimi summary zangu zote jamaa alikuwa anatoa copy, pia kama notes hatupewi alikuwa anachukua zangu, alikuwa anaperform vizuri sana kushinda wasiosikia muda mwingine anapona sisi tukiwa tunafanya make-up.....chamuhimu alikuwa na lecture mmoja aliemzoea sana akamuweka wazi shida yake so hata akiharibu kwa lecture mwingine basi huyu lecture wa karibu anamtetea au kumsaidia......
Nje ya masomo alikuwa anajitenga sana, ila alikuwa anajumuika mara moja moja na sijui huko kwao, pia aliajiriwa tulivyomaliza chuo, kati yangu na yeye na group letu yeye alikuwa wakwanza kuajiriwa sehemu nzuri tu, na kwamujibu wake alipata nafasi bila connection.....
Jiamini usitumie muda mwingi kujitesa kufikiria tatizo lako.....ufanye maongezi ya lazima mengine yasiyo ya lazima yapotezee tu mkuu.....pia jamaa alikuwa na kifaa cha masikio wanaita Hearing aid ila hakuwa anakivaa kwa mujibu wake alisema kinamsababishia uwezo wake wa kusikia kupungua yani hivyo vifaa vinaongeza sauti hivyo zinamchanganya..... Mungu akusaidie