Miji yetu ni very frustrating sana, sehemu ya kupumzikia tunawapa wenye pesa kujenga.
Hizo sehemu zinatakiwa ziwepo wazi kama mdau hapo juu alivyosema ili matajiri na masikini waweze kukutana, saizi inakuwa kazi ngumu kumpata binti wa tajiri wakaoana na kijana kutoka familia zenye maisha ya chini kidogo kwa sababu za kibaguzi kama hizo. Kuoa mdosi nako ni kazi, kidogo waarabu unaweza pata kama unajuhudi vinginevyo upige kitabu upate kikazi ndo umpate kimwana naye opportunist mwisho wa siku unabaki mdomo wazi.
Na hata kupata sehemu iliyo karibu kwa ajili ya kupumzika tu ni ngumu, kila sehemu ukipita katikati ya jiji inanuka mikojo, vinyesi, takataka na majitaka.
Manispaa/Majiji zet/yetu wana urafiki na majiji mengi duniani lakini sijui wanaendaga kuzubaa au kuuza hizi fukwe! Lol, bongo noma jamani kila mtu anavutia kwake anavyoweza mwisho wa siku anabaki zero. Utasikia tu oooo fukwe za kawe zinamilikishwa kwa mwekezaji oooo, unajua alikyekuwepo kashindwa kazi, sababu kibao bila tija. Katiba jamani tuipiganie.