SUZAN KIWANGA SUZAN- mwanamke mwanaharakati wa ukweli ninayemfahamu, ndiye aliyenipokea kwenye MWENDELEZO WA harakati zangu 2004 somewhere na kunipa mwongozo wa wapi nianzie hadi leo nifumbapo macho nakumbuka siku ile, nimemtazama bungeni leo anamshukia ...spika, katika hoja ya Elimu anasema serikali inadhalilisha usomi, ni kweli amedokeza kuwa posho za kujiimu za wanafunzi wa elimu ya juu ni ishara ya kuwa serikali haina dhati ya kuwasaidia wanafunzi hawa, na tena inawafanya waingie kwenye mitego na kuambukizwa ukimwi, akasema kuwa enzi za mwalimu hali haikua hivi, MARA Spika anamkatisha na kusema kipindi hicho wanafunzi walikuwa wachachee, Mama Suzan anamjibu kuwa ''ni kweli walikuwa wachache lakini hata pesa zilikuwa chache, kipindi hicho nchi haikua na wawekezaji kama sasa''....hahahahaaaaa Na wewe uwe mbunge wa jimbo sasa!!!! kiwango chako si cha viti maalum!!