Jamani anataka kufia bungeni huyu tumwokoaje??



Mwacheni huyu mzee. Kusema kuwa amefulia si sahii,Mrema, ni haki yake kikatiba kugombea. kwani wako viongozi wengine wa vyama vingine tangu kuanza kwa uchaguzi wa vyama vingi wana gomea nafasi ya urais lakini hawajafanikiwa.
Mimi naona watu sahii wa kusema huyu mzee hafai ni wapiga kura wake. Kama wanchi wa jimbo lake wanamkubali, basi agombee ubuge. Sisi hatuna sababu sana ya kumjudge. Bungeni wapo wabunge wazee kuliko yeye, na bado wanaendelea kuwepo bungeni,na chama tawala kinaendelea kuwaweka hata kama hawakuchaguliwa na wananchi, basi wanateuliwa.
 
Kwa taarifa yenu wapiga kura wa jimbo la Vunjo bado wanamkubali sana Mrema kutokana na rekodi ya maendeleo aliyowaletea akiwa mbunge wao miaka kumi iliyopita.

Mnaposema kafulia ati hakufanya ufisadi hapo nawashangaa manake mnajichanganya, hamueleweki mko upande gani.

Mrema ameonyesha mfano wa mwanasiasa wa ukweli, anasimamia kile anachokiamini. Akiwa ccm alipanda sana hadi kufikia naibu waziri mkuu, lakini alipoona hawezi kubadilisha usanii wa chama hicho aliondoka na akakubali kuachia maslahi aliyokua anapata. Aliukataa ufisadi kwa matendo tofauti na wapiganaji waliopo sasa.

Afya ya Mrema haionekani kunawiri lakini sio sababu ya kusema ati ataenda kufia bungeni. Kwani ni wabunge wangapi wameanguka mjengoni na hata kufa, hiyo sio sababu. Anaona anaweza na amejitolea kwenda kuwatetea wananchi wake hata ikibidi kufia huko. huo ndio uzalendo, mwacheni.

Karibu mjengoni mzee wa Kiraracha na anaeweza kupambana na wewe aje Vunjo tumuaibishe.
 
Naona yuko sawa kabisa kwani maisha ya bongo siasa ndo inalipa,msishangae kumwona mkapa naye akitaka kugombea huko nanyumbu,siasa za bongo ni upumbafu mtupu!
 
Naona yuko sawa kabisa kwani maisha ya bongo siasa ndo inalipa,msishangae kumwona mkapa naye akitaka kugombea huko nanyumbu,siasa za bongo ni upumbafu mtupu!

hahaaa, sawa na yule ex-mkuu wa majeshi alipoliaibisha jeshi kwa kugombea!!! yaani siasa inakuwa juu ya ukuu wa majeshi!!

Yes kuna haki ya kikatiba, but wait! Huyu mrema watampima afya kwanza??
 

Mkuu good observation and nice of you to be objective but you are living out something important. Mshahara wa ubunge halafu na uwaziri unamtohs kabisa mtu kutajirika kihalalai. Hawa viongozi wetu wanaoiba siyo kwamba mishahara na bonus mbali mbali hazi watoshi bali ni wao hawa ridhiki. Haingii akilini mtu aliye kuwa mbunge kwa miaka ishirini mpaka kufikia kuwa naibu waziri mkuu asiwe na pesa na vitega uchumi kisa hakua mwizi. Sasa kama yeye hali yake ni hivyo je wafanya kazi wengine wa serikalini ina kuaje?
 
Ivi hana washauri?
Jamani nasikia eti mama simba alishawai kwenda south kutibiwa maradhi ya kichwa?
 
Lyatonga, tunakumiss bungeni, naamini utarudi tu, maana Wanavunjo wameamua moja, kupeleka jeshi mstaari wa mbele, narudia jambo moja la hakika, A.l. Mrema atashinda uchaguzi ujao. kama mnadhani inahitaji falsafa za kiona mbali kujua hili basi mmepotoka.
mwingine ninayemmiss bungeni ni Thomas Nyimbo, Mbowe,
 
Lyatonga mrema nadhani sasa anaumwa kichwa... yaani pamoja na maradhi yote anaamini anaweza kuwakilisha wananchi?!!

Kwani kuwa na maradhi ndio kushindwa kuwawakilisha wananchi?
Ugonjwa si kifo babu weee
 
Kwani we ulitaka afie wapi?mwenzako amepiga mahesabu anataka kufia bungeni ila azikwe vizuri kwa heshima kama mbunge na mwanasiasa Mkongwe.Anataka kurudisha hadhi yake kwa kipindi kifupu kilichobaki cha maisha yake.
 

Mvina
Mrema wala hahitaji kuboresha maisha yake kwani anafahamu kwamba ana muda mfupi sana wa kuishi hapa duniani.Anataka kuwa Mbunge ili azikwe vizuri na si vinginevyo.
 
Jamani,ebu tuangalie upande wa pili wa shiliingi,
We voted for this guy mwaka 1995 tena majority votes na aliweza itikisa CCM kwa mara ya kwanza.I can declace kua this guy was good tena sana tu lakini wat happened to him ni makucha ya CCM,CCM crippled him politically,walimuua kisiasa,walipenyeza majungu kipindi kile NCCR halafu TLP hii yote ni kuhakikisha kua wat happened 1995 hakitokei tena,
in short walimuangamiza kabisa,n now here he is,AMEFULIA but coming to another side hyu jamaa kipindi akiwa Waziri tunakumbuka kash kash yake,lets not spit on him but look on wat really happened mpk akawa hapa alipo.
Let him get tht MP thing,tumpe nafasi tena myb he will rise up with smething,n by the way if we can give it CCMz why nt try this guy too?
 

kumbuka umri na afya yake na ujue hata kingunge kuna wakati alikuwa na busara kabla hajapa ugonjwa wa uzee
 
Bora ya Mrema kuliko Kimaro anaejifanya kupambana na ufisadi wakati hakuna lolote alilowafanyia wananchi wa Vunjo
 
Mwacheni kumsimanga mwingine, kama imekuboa kachukue fomu na wewe ugombee. Alaa
 
Kufia bungeni,si ndio atazikwa na dola,huko TLP mzikaji nani,njaa tupu.
mwaacheni agombee kwani ni haki yake,si mtanzania.Tatizo ni nini,mbona na mimi nataka kugombea kwetu Kyela,mwakyembe kaa mkao wa kula.
 
Acheni kukufuru Mungu, wangapi wazima na wanakufa wanaacha wagonjwa?

Mrema wala hahitaji kuboresha maisha yake kwani anafahamu kwamba ana muda mfupi sana wa kuishi hapa duniani.Anataka kuwa Mbunge ili azikwe vizuri na si vinginevyo.

We nafikiri ni mgonjwa kuliko mrema. Maisha ya Mrema ni bora kuliko unavyofikiri, na sio kila mwana siasa anafuata kipato bungeni. Wapo kina , Ndesa, Mkono, Silaa na wengine wengi wanaliopo pale kwa sababu wanataka kusimamia kile wanachokiamini. Na hiyo ndo siasa.
 

Mazishi yake yalifanyika wapi ?.Wapiga kura wa Vunja waachwe waamue nani wanataka awe mbunge wao 2010.


Malecela alishakuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais.kwa sasa ni mbunge wa Mtera tayari katangaza atagombea tena 2010 mbona hakuna kelele!!!!!.Mzee wa kiraracha katangaza atagombea mnaaza fitina zenu wakati mnajua waamuzi ni wapiga kura wa Vunjo.


embu nisaidien analipwa ngapi kama pension kwa mwezi??

General Mboma analipwa pension kiasi kwa mwezi mbona alichukua fomu za kugombea ubunge.Mrema kama analipwa pension ndogo au kubwa bado si kigezo cha kumyima haki yake ya kugombea ubunge.


Tuko pamoja muze tunamhitaji sana Mzee wa Kiraracha pale mjengoni.
 
Wana saikolojia wansema sisi wote kama binadamu tuna kichaa. Kila mtu ana kichaa chake fulani tangu anakua mtu mpaka unakufa. Mrema ana ukichaa wa kupenda madaraka. Ndio kichaa chake!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…