Jamani akiba yangu yote imekombwa tigo pesa, nifanyaje?

Lofawamali

JF-Expert Member
Jun 9, 2014
304
146
Habari za jioni wanajamvi,

Akiba yangu yote imekombwa tigopesa nifanyaje?Nimejaribu kufatilia lakini naona maruweruwe nimeambiwa niende polisi kutoa loss report wamenipa R/B.

Nilipofika tigo msimbazi kupeleka malalamiko wanadai ni common issue na kesi za sampuli hiyo zimekua nyingi no any help wat should i do?Na nina uhakika wa namba ya siri kutokua exposed kwa mtu yoyote yule nawa guarantee kwa hilo.

Je kuna mtu ameshawahi kukutana na tatizo hilo?

Karibuni kuchangia mawazo
 
Unavyoongea inaonekana hauko serious, pesa imetolewa kwa wakala gani? Mtafute then kamata, au zimetumwa kwa nani? Mtafute kamata!
 
Pole sana... Ni kweli kesi kama hizo zipo nyingi.. inaonekana mitandao ya simu imeshindwa kudhibiti wizi wa fedha kupitia mtandao..

Pole sana... Siku hizi hizo huduma za mitandao yote hazipo salama kabisa. Ukiweka pesa tumia hapo hapo au tuma hapo hapo usiache kabisa kwa muda mrefu unakuta haipo...
 
Unavyoongea inaonekana hauko serious, pesa imetolewa kwa wakala gani? Mtafute then kamata, au zimetumwa kwa nani? Mtafute kamata!
Chief niko serious nimeenda makao makuu wamentolea kop ya miamala yote recently na pesa ya mwsho ambyo imepotea inaonekana namba ambayo haipo hewab kabisa ni serious issue..
 
Pole sana... Ni kweli kesi kama hizo zipo nyingi.. inaonekana mitandao ya simu imeshindwa kudhibiti wizi wa fedha kupitia mtandao..

Pole sana... Siku hizi hizo huduma za mitandao yote hazipo salama kabisa. Ukiweka pesa tumia hapo hapo au tuma hapo hapo usiache kabisa kwa muda mrefu unakuta haipo...
Sure chief nakubaliana na wew kabisa bila hata kipingamizi..
 
Chief niko serious nimeenda makao makuu wamentolea kop ya miamala yote recently na pesa ya mwsho ambyo imepotea inaonekana namba ambayo haipo hewab kabisa ni serious issue..
hapo ni wizi profesional yaan watu wako vizur ukienda wanakupa muamala wa mwisho kuutoa ujue wakala gan katoa hio pesa ila kuna mchezo wa wizuliobarikiwa ba viongoz w a makampun kwa mfano ukitumiwa pesa huion but ukienda kulalamika unatumiwa hapohapo bila maelezo ya kilichotokea
 
Dah wameniweza kwel wamekula hadi kuku wa dawa....
 
Chek na TCRA pia maana usalama wa mifumo ya
kifedha kwa njia za simu inawahusu.... na je hao walio chukua wamezitoa kwa wakala kwa kutumia password yako wau ni watu wa tigo?
 
Wekeni fedha benki. Hii mitandao itumike tu kutuma na kupokea fedha.
Hili neno la msingi.
Ila hii pia inaweza kuwa sabotage inafanywa kwa makusudi na wafanyakazi hasa watu wa IT kwa kukomoa Kampuni zao.
Naamini kabisa kwamba Kampuni nia zao ni nzuri sana na zimetusaidia saana,ila kuna wafanyakazi hasa wa IT na baadhi ya Managements za Kampuni hizi kula rushwa na Banks ili waonekane Kampuni za simu sio Salama kwa Pesa zetu.
Hili ndio mie naliamini saana,ila kampuni za sim nia yao ni Nzuri ila wao kwa wao ndio wanafanya sabotage kwa kula rushwa kutoka kwenye Banks baada ya banks nyingi kuanza kudorora.
Hili ni Zaidi ya Jipu.
Makampuni ya sim lazima mjipange na mjue kwamba na sie wateja tunajua mnachokifanya,wenzenu ulaya walishtakiwa kwa uzembe huu na kukaribia kufilisiwa kwa tamaa na faida za wangine.Ongeeni na Njaa zenu.
 
Nenda TCRA kawaripoti watakurudishia fedha zako, pia kusanya risiti za safari yako mpaka tcra pia udai watakulipa na usumbufu wako, usiwaachie kuna makampuni hushirikiana na watanzania wasio waaminifu kulihujumu taifa letu na kulipa sifa mbaya, hivyo bora ukatetea hili na kulisambaza mitandaoni.
 
Ntaenda kwa kwel kama ndo hvyo mana ni tabia ambayo inakithiri kila kukicha...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom