Unajua siku za huko nyuma bodaboda zilizuiwa kabisa kutumiwa kwa kubebea abiria. Na pia utaratibu wa matumizi yake ulikuwa unadhibitiwa sana katika maeneo ya mijini. Lakini wakati wa kampeni za uchaguzi, CCM walizinunua kwa wingi na kuwapa vijana wa kuwasaidia kwenye kampeni, na hata wale walioamua kuzitumia kwa biashara, hawakuwazuia kwa kuhofia kwamba watakosa kura kutoka kwa vijana hao. Na kwa kuwa waliziruhusu, hivi sasa wanaona shida kuzizuia tena. Tutaisha kusema ukweli. Katika nchi inayoongozwa na serikali chovu kama ya Kikwete huwezi kutegemea aina yoyote ya suluhu ya matatizo ya wananchi.