Jakaya ni rais wetu wote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jakaya ni rais wetu wote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Taifa_Kwanza, Mar 3, 2011.

 1. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Siku za sasa kuna upoteshaji mkubwa sana wa hali halisi ya uongozi katika Taifa wetu unafanywa na makada wa CCM na/au watu fulani wenye imani ya dini ya Kiislamu kwamba Watanzania tunapoelezea kutoridhishwa kwetu na utendaji wa serikali yetu wao wanakimbilia kudai kwamba malalamiko hayo yanaelekezwa kwa Muislamu mwenzao.

  Sasa naomba nitoe tamko binafsi kwamba watu hawa ni wakupuuzwa na kutosikilizwa hata kidogo sababu misingi ya hoja zao haina mashiko, ni wachochezi wa kidini na ni ushahidi wa kwamba watu hawa na wote wanaokubaliana nao wana mapungufu makubwa sana ya uelewa wa imani za kidini na maswala ya utawala hasa katika ngazi ya kitaifa.

  Jakaya Kikwete ni Rais wa Watanzania wote, wakati anapata fursa ya kuliongoza taifa letu kwa mara ya kwanza alichaguliwa na watanzania kwa wingi wa kura za hali ya juu sana. Wakirsto na wapagani walimpigia kura. Hakuna kikundi chochote chenye haki ya kumtetea wala kumkingia kifua Kikwete wakati watanzania wanamuhoji au kumlalamikia kwamba anatuongoza vibaya, Si CCM, si wakwere, si ridhiwan, miraji wala mke wake anayeweza kusema tunamuonea baba yao, mwenyekiti wa chama chao wala ndugu yao kwa sababu tu tunachuki na vikundi hivyo.

  Asimame Muislamu mmoja tu, atueleze kwamba ahadi alizozitoa Jakaya wakati wa Kampeni zake alikuwa akizitoa kwa Waislamu pekee, na watanzania woooote watakaa kimya. Lakini kama alitoa kwa watanzania basi ni lazima awajibike kwetu.

  Ugumu wa Maisha unatusumbua watanzania wote, ukali wa matatizo ya umeme ni mwiba kwa watanzania wote, Hakuna Muislamu hata mmoja anayepata nafuu sababu ya uislamu wake katika hili. Waislamu mchague moja kutumika katika kipindi hiki cha mpito kutoa hisia za ahueni kwa chama cha mapinduzi ama kufuata dhamiri zenu za kweli juu ya hali halisi ya uongozi wa nchi yetu.

  Kama Jakaya angekuwa anahujumiwa kwa misingi ya kidini, Mwakyembe asingemtoa Kafara Mkirsto mwenzake Lowasa katika kashfa ya Richmond na Kumfichia siri Muislamu Jakaya. Kama DR Slaa angekuwa mdini asingeshadidia uchafu wa Deep Green, Meremeta wala kiwira ambazo ni mizigo ya mkirsto mwenzake Benjamini Mkapa, asingemlazimisha Jakaya kumfukuza kazi mkirsto mwenzake Gavana Balali,

  Watanzania hawataka kata tamaa hata mara moja katika kuhakikisha Jakaya Kikwete anatulia na kufanya kazi aliyoiomba, na akaibinafsisha kwa kuisukuma familia yake yote katika kampeni za urais, na kuchakachua uhesabuji wa kura.

  Kwa misingi ya Katika ya nchi yetu, yeye ndio rais wetu, na sasa tunataka utekelezaji ama aondoke.
   
Loading...