Ngamanya Kitangalala
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 501
- 1,214
Moja ya jambo jema la kujifunza kwa wanasiasa wa sasa, kutoka kwa mh Jakaya Mrisho Kikwete, Rais mstaafu wa awamu ya nne
Ni kuheshimu na kukubali pasipo kinyongo maamuzi ya vikao vya chama
Najaribu kukumbuka mwaka 1995, kama ingelikuwa wanasiasa wetu wa kizazi hiki, pengine mh Kikwete leo asingeitwa Rais mstaafu
Pamoja na yote lakini yeye aliendelea kuwa mwanachama mtiifu, pasipo kinyongo wala kulalamika
Nidhamu hiyo ndio iliyompatia fursa ya kuja kuwa mgombea wa chama chake 2005, kisha kupelekea kuja kuwa Rais wa awamu ya nne ya JMT
Hili ni funzo tosha kwa wanasiasa wetu wa sasa, hata kama utaona au kuanini ukutendewa haki na maamuzi ya vikao vya chama chako
Nidhamu na utiifu wako kwa chama chako ni jambo la muhimu sana, kwani itaweza kuwafanya hata hao unaohisi wamekuonea, waweze kubadili mawazo kwa siku za usoni na kukuona ni mtu sahihi kuweza kupata kile ulichokuwa unakitafuta