Jakaya foundation

Jakaya foundation

hendeboy

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
218
Reaction score
21
Mwenye kufahamu zilipo ofisi za Jakaya Foundation anijuze, nimesikia wanatoa mkopo bila mashart. Tafadhali nisaidieni.
 
i can smell a rat..
sio matapeli hao?
 
TAARIFA KWA UMMA
Benki Kuu inapenda kuutahadharisha umma kuwa katika siku za karibuni kumekuwepo na mtandao wa
matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayo Wapka.mobi.
Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayo
inamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia
sekretariat ya Utumishi wa umma ofisi ya Rais.
Matapeli hao wanaeleza kwamba Taasisi hiyo inatoa mikopo ndani ya masaa 24 kwa Mtanzania yeyote
mwenye umri kuanzia miaka 18 endapo atajiunga kwa kulipa ada ya shilingi 37,000/=.
BENKI KUU INAUARIFU UMMA KUWA HAIITAMBUI NA WALA HAIHUSIANI KWA NAMNA YOYOTE ILE
NA TAASISI INAYOELEZWA KWENYE TOVUTI HIYO.
Kwa taarifa hii, Benki Kuu inatoa tahadhari kwa Wananchi kutojihusisha na Taasisi hiyo ya kitapeli kwa
ajili ya kupata huduma za mikopo kama ambavyo inadai.
IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI
BENKI KUU YA TANZANIA
DAR ES SALAAM.
29/5/2013 ...........matAPELI HAO
 
ahsante sana...
 
kwa vile jina la Rais linatumika kutapeli vijisenti vya walala hoi vyombo vya usalama viko wapi? Nchi imekuwa shamba la vilembwe na vilembwekeze, si la bibi tena
 
Hata hivyo ukisoma kwa makini tovuti ya matapeli hawa utagundua kuwa uhariri wa Kiswahili haukufanyika! Pamoja na hayo ni vigumu sana kwa taasisi kubwa yenye jina la Jakaya Foundation kugawa fedha kama njugu, pasipo utaratibu unaoeleweka kisheria, ikiwemo dhamana ya mali. Ni wachovu tu wa akili wanaoweza kutapeliwa.
 
Back
Top Bottom