mchwa mpaka
Member
- Nov 18, 2009
- 35
- 70
Leo niliingia mahakama Kuu Moshi katika usikilizaji wa kesi ya mauaji ya kukusudia ya mwanafunzi wa shule ya Scolastica inayowakabili watu watatu akiwemo mmiliki wa shule, Bwana Edward Shayo. Mimi niliingia kama msikilizaji wa kawaida ila nilichokisikia nimejiuliza mara mbilimbili ni kitu gani kinafichwa na ndio maana nimelazimika kukuuliza mheshimiwa Jaji mkuu, mhimili wako wako unaanzisha malumbano haya na wanahabari ili nini?
Jaji Firmin Matogolo anayesikiliza kesi hiyo amewapiga marufuku waandishi wa habari wanaoripoti kesi hiyo, kuchuchua notes za ushahidi wa mashahidi walioanza kutoa ushahidi leo na badala yake wasikilize tu kama wananchi wa kawaida na kama watahitaji habari waende kwa msajili a mahakama kuu atawapa.
Kwanza kesi hii ni moja ya kesi zenye public interest kuwahi kuonekana na inagusa hisia za wazazi wengi nchini wanaotaka kujua nini kilimpata mwanafunzi Humphrey Makundi mwaka 2017 hadi maiti yake iokotwe mtoni mita 300 tu kutoka shuleni, licha ya kwamba alikuwa shuleni. Si wazazi wote nchin wanaweza kusafiri hadi Moshi kuisikiliza na pia open court isingetosha. Kwa hiyo wengi walitarajia kupata ukweli kupitia media.
Jaji anapowataka wanahabari wasichukue notes mahakamani, watatimizaje wajibu wao wa kuhabarisha umma? Huyo msajili ana ujuzi gani wa kihabari wa kujua vionjo vya habari? Je, muda wote atakuwepo mahakamani na atakuwa tayari kutoa habari saa yoyote mwandishi anapotaka kutoka chumba cha mahakama?
Ninavyofahamu, waandishi wanao cover Bunge na Court proceedings wana enjoy qualified privilege endapo watareport kwa usahihi. Mahakama inataka kusema hata bungeni sasa waandishi wawe wanachukua taarifa kwa Katibu wa Bunge? Kwanini mahakama itake kuendesha kesi hii gizani? Kama mwandishi ataandika ndivyo sivyo si kuna sheria ya contempt of court?. Nitawashaa sana wanahabari, taasisi zao na taasisi za haki za binadamu hawatakaa kimya katika uminyaji huu wa uhuru wa vyombo vya habari.
Jaji mkuu au Jaji Kiongozi, anapaswa kuingilia jambo hili kwani wanahabari wamekuwa wadau muhimu wa mahakama. Leo wanakuwaje maadui?