Jana katika sherehe za kuwatambua na kuwasajili Mawakili wapya pale kwenye viunga vya Law School of Tanzania,Jaji Mkuu wa Tanzania amegusia jambo.Jambo lenyewe ni uhaba wa Mawakili nchini Tanzania. Pamoja na waliosajiliwa jana,Mawakili wa Tanzania nzima hawafiki 3500.
Yawezekana Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman hamjui wa kumlaumu. Mimi namtajia: Law School of Tanzania inayoongozwa na Jaji Dr.Gerald Ndika. Taasisi hii iliyopewa majukumu ya kuwaandaa Wanasheria kuwa Mawakili,imekuwa ikichelewesha mno matokeo ya wanafunzi wake. Matokeo huchukua hadi miezi saba kutoka. Kila mwanasheria hutakiwa kufaulu masomo yote ya Law School of Tanzania ili kuwa na sifa za kuwa Wakili. Masomo hapo ni ya mwaka mmoja.
Ikumbukwe kuwa,kusajili Mawakili wapya hufanyika mara mbili tu kwa mwaka: mwezi Juni na mwezi Disemba. Kama matokeo yanachelewa hivyo,wangapi watawahi miezi hiyo? Iweje vyuo vikuu viweze kutoa matokeo mapema vikiwa na wanafunzi wengi halafu LST ikiwa na wanafunzi wasiozidi 300 icheleweshe matokeo kiasi hicho? Jaji Mkuu amemuona sasa wa kumlaumu? Jaji Mkuu na LST waache porojo,wafanye kazi!