Jaji Mkuu Chande atoa siku 7 kwa mahakimu 508, watoe maelezo kwa nini wasifunguliwe mashtaka

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
JAJI Mkuu wa Tanzania Othuman Chande ametoa siku saba kwa mahakimu 508;watoe maelezo ni kwanini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na kuwajibishwa, baada ya kufanya kazi chini ya kiwango.

Jaji Chande ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Sheria.

Alisema kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ni 250, ambapo Mahakimu Wakazi 121 kwenye mahakama hizo wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.

Alibainisha kuwa kiwango cha kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ni 260, ambapo mahakimu Wakazi na Mahakimu  wa Mahakama za Mwanzo 387 wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.

Ukiondoa wale ambao wameajiriwa karibuni, wanaofanya kazi kwenye mahakama za mwanzo zisizokua na mashauri mengi au waliyokwenda masomoni kati kati ya mwaka  au likizo za ujauzito hawatahusika katika sakata la kujieleza.

Majaji Wafawidhi nimewaagiza wachambue na kuanisha mahakimu wote walioshindwa kufikia kiwango cha kesi walizopaswa kuamua kesi 250 na kesi 260 kwa mwaka jana na kuwataka watoe maelezo ndani ya siku saba kwa nini wasichukuliwe hatua," alisema Jaji Chande

Jaji Chande alitoa muda wa kukamilika kwa mchakato huo, ambapo walizitaka idara husika ndani ya siku 21 kila kitu kiwe kimekamilika ili ijulikane ni hatua gani wanachukuliwe.

Mahakama haikubali hakimu ambaye anabembeleza kesi. Hakimu hatakiwi kufanya hivyo anatakiwa asikilize kesi hizo naazimalize. Haiwezekani katika mahakama moja hakimu mmoja anamaliza kesi 800 mwingine anamalizia chini ya 100  hilo halitakubalika kutokana na kasi ambayo tunayo," alisema

Jaji Chande alisema mahakimu hao watapelekwa katika kamati zao kwa hatua ya kujieleza. Kazi kuu ya kamati hizo ni kupeleleza, kuchunguza na kushughulikia mashtaka yote ya nidhamu ya mahakimu.

"Mahakimu wote walioshindwa kufikia malengo ya mwaka la kesi na kushindwa kutoan sababu za kuridhisha kwa nini wameamua idadi ndogo ya kesi kuliko walivyopaswa, ambapo itashughulikiwa haraka na Kamati za Maadili za Mahyakimu kwa mujibu wa sheria na taratibu za haki," alisema

Hata hivyo, Jaji Chande alitoa pongezi kwa mahakimu ambao wamevuka kiwango, ambapo mahakimu 14 wameamua zaidi ya kesi 700 kwa mwaka jana na mahakimu wengine wamesikiliza kesi 915,789 na 778.

Alisema mkakati wao ni kuanza kesi sifuri mwaka unapoanza, kwa sababu kuna baadhi ya mahakama za mwanzo zimekuwa zikimaliza kesi na kuanza mwaka upya.

Jaji Chande alisema Januari 1, 2015 mahakama za mwanzo zilianza na kesi 34,126 na mwaka huu Januari 1 zilianza na kesi 20,431. Kiwango cha kumaliza kesi ukilinganisha na idadi ya kesi zilizosajiliwa 2015 nni zaidi ya asilimia 100. Mahakama ya Mkuranga asilimia 141, Rufiji asilimia 121 na Bukoba Mjini asilimia 224.
 
Nafikiri sababu kubwa ya kushindwa kufikia malengo hayo inatokana pia na kucheleweshwa kwa kesi kutokana na upelelezi kutokukamilika kwa wakati,kwasababu hiyo na polisi nao wahusishwe katika hili.
 
Kuna kesi zipo mahakamani miaka 20 sasa hivi. Lakini vile vile mawakili wanatakiwa kulaumiwa vilevile.
 
Washughulikiwe maana rushwa mbele kuliko kazi
 
I hope sio siasa, wala matamko ya kila siku.

Wengi wamedhulumiwa kwa kesi kucheleweshwa..
Ni wakati muafaka sasa haki zitendeke na kesi zitolewe hukumu kwa wakati. ......
 
Hata kama ushahidi haujamilika kanyagatwende ili kupata kumaliza kesi nyingi na kupongezwa
 
Tatizo sio kuchelewesha kesi ,kuna kesi ambazo hazistahili ata kufika mahakamani zinaweza maliziwa kwenye kata tatizo ni mfumo kila jambo mpaka liende mahakamani.
 
Mlala hoi ndiyo anaonewa katika mahakama zetu.

Hana uwezo wa kutoa rushwa ili apewe dhamana.

Hana uwezo wa kulipa dhamana.

Watu wanateswa na kupigwa na Polisi ili wakubali makosa kinguvu.

Kama Raisi anaheshimu haki ya binadamu, angewasamehe watuhumuwa wote waliofungwa zaidi ya miaka mitatu kusubiri hukumu zao, hasa walio na makosa madogo madogo.

Bora, wangepewa kifungo cha nje au kuamriwa wasafishe mji kama adhabu.

Jela ibaki kwa wauaji, mafisadi na majambazi waliotumia silaha.
 
Haki ikiharakishwa sana pia inakosa viwango,tutarajie kesi kufutwafutwa au watu kufungwafungwa bila sababu ili hakimu afikie idadi ya kesi,,hilo nimelishuhudia mwenyewe,pia kesi za jinai zinakwamishwa na upelelezi na mawakili
 
Na maslahi yao vipi!? Mnataka kazi ifanyike lakini anakula na kulala wapi huyo hakimu kimya. Ok ngoje hukumu zisizo na kiwango zianze kumiminika. Kwa mimi watu wa kuwekewa ultimatum ya ukweli ni majaji, kwani wao maslahi yao ni bora sana; mshahara wao na marupuru na safi, shangingi la kutembelea lipo saa 24 kwa ajiri yake, nyumba wanapewa na serikali, na kama nyumba hamna wanawekwa hotel ya nyota tano mpaka nyumba ipatikane. Ila kwa mahakimu ni dhiki kuu.
 
Nilijua ameamua kuingia kazini kumbe anaadhimisha siku ya sheria, this does not count responsibility kabisa, ningemuona anatija kama angesema amekwisha wachukulia hatua tayari
 
Nafikiri sababu kubwa ya kushindwa kufikia malengo hayo inatokana pia na kucheleweshwa kwa kesi kutokana na upelelezi kutokukamilika kwa wakati,kwasababu hiyo na polisi nao wahusishwe katika hili.
Mkuu sheria inataka upeleleze uishe ndani ya siku 60.kama bado hakimu anatakiwa kuitupa kesi
 
Back
Top Bottom