MASIKIN JEURI
Senior Member
- Jan 31, 2013
- 134
- 22
Safi sana Jaji Boman, tunapenda viongozi wasiokuwa wanafiki kama wewe, eti serikali mbili za nini sasa! tuwe na serikali tatu, na Tanganyika yetu ijulikane hivyo
IBARA YA 1 YA RASIMU YA KATIBA YENYEWE
1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.
Hivyo ndivyo inavyosomeka rasimu yenyewe. Kama jina la Zanzibar limebaki, na kama nchi zote bado ni huru, kwanini jina la Tanganyika life?
senkiyuu veri machi !!!!!
Mimi kwangu serikali mbili tosha ili mradi kero za kweli zirekebishwe kwa katiba. Wanaoratibu madai ya serikali 3 zenj hawana nia njema. Wanataka serikali ya tanganyika kama hatua ya kuvunja muungano. Sasa kwa nini tupoteze tena muda badala ya kutafuta maendeleo kwa kupigiwa kelele za kero ya muungano wakati wazenj wanawasikiliza wenye nia ya kuuvunja. Suluhisho la kweli ni kua na serikali moja au mbili vinginevyo muungano uvunjwe sasa.Tupeni ghrama (figures) za serikali 2 na tatu kisha tuchambue na kupembua. Naona neno "mzigo/ghrama" linapigiwa upatu sana. Kwangu mimi kama ndio gharama ya kulipa ili tuwe na amani na maendeleo I will happily pay. Kumbuka "cheap is always more costly/expensive"