Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Jaji Mabel Jansen wa Afrika kusini amenukuliwa akisema kuwa, ubakaji ni sehemu ya utamaduni wa wanaume wa Afrika na ni kitu ambacho wanakifurahia sana, na pia hajawahi kukutana na msichana mweusi ambaye hajabakwa.
Wananchi wa Afrika Kusini wamechukizwa sana na wameazimia kuandamana wakitaka Mabel Jansen afukuzwe kazi. Wanaharakati wa Afrika ya Kusini pia wameeleza kuwa maneno hayo yamewavunjia heshima wanaume wote barani Afrika.
Hali hii imetafsiriwa kama ubaguzi wa rangi kwani hawakufurahishwa na kitendo cha jaji huyo kutumia rangi ya ngozi kuwagawa watu. Suala la ubaguzi wa rangi Afrika Kusini lilitawala sana enzi za ukoloni kitu kilichopelekea watu weupe kupewa uhuru wao mwaka 1910 huku watu weusi wakizidi kutumikishwa na ilipofika mwaka 1994 ndipo kwa mara ya kwanza watu wote waliruhusiwa kushiriki uchaguzi.
Gillian Schutte ambaye ndiye aliyeweka hadharani maneno ya jaji huyo alisema amefikia uamuzi huo kwani jaji huyo yupo katika nafasi ya kufanya maamuzi sawa kwa watu wote lakini inaonekana anawachukulia watu weusi kama wanyama na mijitu isiyofaaa.
Mtayarishaji huyo wa filamu nchini Afrika Kusini Schutte alisema ameweka hadharani hilo hata kabla ya hapo alishautuma ujumbe huo kwenye vyombo vya habari na kwa baadhi ya mawakili nchini Afrika Kusini.
Mabel Jansen aliyasema maneno hayo alipokuwa akiwasiliana na Gillian Schutte kupitia mtandao wa facebook.
Source: swahilitimes