Wanabodi,
Vyama vikongwe afrika vingi vilishasambaratika mfano nzuri KANU.
Kwa Tanzania huu ni mwaka wa 51 CCM bado ni chama ambacho hakijasambaratika. Unaweza kusema kina matawi kuanzia ngazi ya shina au nyumba kumi, rasilimali za kukiendesha au ni chama chenye dola. Vyovyote unavyoweza kukitetea utajikuta kwenye lindi la fikra zinazokinzana nawe vilivyosambaratika vilikuwa bora na sababu uwezo wa kuendelea kuliko ccm iliyomeguka vipande vipande kama vile ccm ya wasionacho, ccm ya wenye uwezo, ccm ya familia na viongozi, ccm mtandao, ccm ya wazee, ccm ya wasaliti, ccm asilia ya wakulima na wafanyakazi na ccm bendera fuata upepo maslahi mbele au ccm mkono mtupu haulambwi na ccm mwaga pesa upate kula bado CCM imeendelea kuwepo pamoja na hayo.
Huku vyama vingine vikisambaratika kirahisi kama moto wa karatasi bila migawanyiko ya kuanzisha chama ndani ya chama kama nilivyoeleza.
Jamii forums kisima cha mjadala Wana jamvi hebu tujadili jins ya kuisambaratisha siku nyingine tutajadili kuihuisha kuimarisha.