gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,305
- 3,327
Kwanza kabisa nianze kwa kukiri juu ya umuhimu wa upinzani nchini,
Ili tanzania isonge mbele licha ya serikali imara kama iliopo sasa, tunahitaji upinzania imara na madhubuti.
Lakini kwa hali ilivyo sasa ni wazi upinzani wamekosa hoja yakusimamia badala yake wamebaki kudandia hoja zenye kuwaangamiza wenyewe jambo ambalo ni hatari kutokana na umuhimu wa upinzani nchini.
Julius Mtatiro ni mwanasiasa mahiri tena mwenye uzoefu wa muda mrefu lakini kwa namna ambavyo anaenenda sasa anapaswa kukumbuka kwamba upinzani bila viongozi mahiri utakufa.
Jana kwenye ukurasa wake wa facebook mara tu baada ya mh rais kutengua uteuzi wa mh mkuu wa mkoa wa shinyanga mama Anne Kilango mh mtatiro ameandika kuonesha kutetea akidai licha ya uzembe uliofanywa na mkuu wa mkoa lakini hatua alizochukuliwa hazikua sahihi.
Mimi nataka niwakumbushe wapinzani watambue kwamba ile akili walioitumia kumpokea lowasa kwa dhana kwamba nyuma yake anawatu wengi,kwa sasa wakiifanya kwa dhana ileile watakua wanajiangamiza wenyewe.
Kwa sasa mtu pekee mwenye wafuasi wengi nyuma yake ni rais Maguguli na yeyote atakayekua kinyume naye atambue atakua kinyume na kundi lote lililopo nyuma ya raisi.