"J.Cole Apologizing Was The Best Move he Did his Entire Career"

Feisal2020

JF-Expert Member
Nov 15, 2018
786
1,705
Kuna uzi upo humu jukwaani tulikuwa tunabishana na majamaa kuhusu hizi diss tracks zinazotolewa na Kendrick Lamar na Drake. Hii bifu tunaoifaidi vizuri ni sisi tusio mashabiki wa Kendrick wala Drake. Mashabiki wa Kendrick watasifia tu Euphoria kuwa diss track kali lakini ukiwa serious huwezi kutokuiona kama lullaby (diss haiwi soft vile aisee), ukiwa shabiki wa Drake utabisha tu kwamba Meet the Grahams sio diss track kali! Kwa staili hiyo ule uzi watu hawawezi kukubaliana kitu.

Katika kubishana huko kuna member anajiita MastaKiraka akasema “J.Cole apologizing was the best move he did his entire career"! Nilipouliza kwanini akasema "ingekua mwisho wa kazi yake ya kisanii” nilishtukaa!
Member mwingine wa kuitwa George Betram akaongezea, “Yeye mwenyewe J.Cole anajua ambacho kingemkuta, ndo maana akaamua kurudisha mpira kwa golikipa. Labda kama wewe unajua uwezo wa J.Cole kuliko anavyojijua unaweza kusema vinginevyo"... Yani kwamba J cole aliomba msamaha akisema “Kendrick Lamar nisamehe bwana najua siwezi kubato nawewe uwezo wangu mdogo kukuliko” au maneno mengine lakini yenye maana sawa na hayo?!!

Shida ya watu wengi tunawapenda sana wasanii kabla ya kupenda game kwanza, matokeo yake tunakuja kuwachukia wasanii fulani wengine kabla hata hatujawasikiliza. Nilitaka kuwajibu MastaKiraka na George Betram kwenye ule uzi lakini majibu yangu yanatosha kuwa uzi mwingine, ninyi na wengine wenye mtazamo kama wenu mtasoma hapa.

Kwenye 7 Minutes Drill Cole anasema,
“Your first shit (Good Kid, m.A.A.d City) was classic, your last shit (Mr. Morale & The Big Steppers) was tragic/ Your second shit (To Pimp A Butterfly) put niggas to sleep, but they gassed it/
Your third shit (DAMN) was massive and that was your prime..

Licha ya kwamba ameonesha kuzikubali DAMN na Good Kid Maad City, pia ameidiss Mr. Morale & The Big Steppers na amesema To Pimp a Butterfly ilikua overhyped!

Tofauti na wanachofanya Kendrick Lamar na Drake saivi (kuchafuana kwa kila mtu kumsemea mwenzie mambo ‘too personal' hadi kugusa familia), Cole alidiss catalogue (albums) na ukubwa wa Kendrick Lamar kwenye game jambo ambalo nalo anakuja kukiri kwamba alikosea, ilimbidi kuongea vitu ambavyo hata yeye haviamini for the sake of diss song lakini baadae his true self won na akayarudisha maneno yake! It takes a man kujua kwamba umekosea, kukubali kwamba umekosea na zaidi ya yote kukubali kuwa responsible kwa makosa yako na kuomba msamaha ukigundua umefanya kosa, wengine huwa tunashindwa kuomba msamaha kwa watoto tukiwakosea, J Cole alifanya mbele ya watu zaidi ya 50K waliokua kwenye ile festival!

Kwenye hizi diss tracks Drake ametuambia kuwa Kendrick huwa anampiga mkewe, kwamba mtoto mmoja wa Kendrick sio wake bali mkewe alichepuka, Dot mwenyewe kwenye Meet The Grahams amewahusisha family members wa Drake (Verse ya 1 anaongea na Adonis-mtoto wa Drake-kwamba akimuangalia baba yake Adonis, yani Drake, anatamani babu yake angevaa ndomu ili Drake asizaliwe), pia kwamba Drake ana pedophile (anapenda kufanya mapenzi na vitoto vidogo), ana gambling addiction n.k!

Hivyo vitu wanavyosemana, haijalishi ni vya kweli au wameamua tu kuchafuana… sio vitu ambacho mtu mwenye akili timamu atapenda kuvishabikia. Haya mambo yanaenda yanakua personal hivi hatujui yatafika wapi, yanaweza ku escalate yakawa makubwa zaidi watu wafanyaje kama Pac na BIG kisa a lame a$$ rap battle na Cole ni mtu smart sana kujua hilo akaamua mambo yasiwe mengi, J.Cole ni mtu ambae hata ngoma zake zimejaa themes kuhusu familia, umaskini, upendo, gun violence, self growth, ubaguzi wa rangi n.k. Cole hasifii mademu,pombe, madawa, macheki,magari ya kifahari na vitu kama hivyo.

Diss tracks zilitakiwa kuwa zina question rap skills za mtu, ubovu wa albums & mixtapes na vitu kama hivyo…kitu ambacho J.Cole alikifanya kwenye 7 Minuter Drill japo anakiri kwamba alisema vitu tofauti na anavyoamini kuhusu Dot kwa sababu ya external influence.

Cole aliomba msamaha kwa sababu ya namna anavyojisikia baada ya kumdiss Dot, sio eti kwa sababu ya kuogopa kuwa Dot anamzidi kuchana na atamfunika. Labda nyie wenzangu mniambie ni maneno yapi hapa mliona yakimaanisha hivyo;

“ I was conflicted because, I know my heart and I know how I feel about my peers, these two n**gas that I’m blessed to even stand beside in this game and let alone chase their greatness. I felt conflicted because I know I don’t really feel no way. But the world want to see blood… I moved in a way that, spiritually, I feel bad. That was the lamest, goofiest sh*t… I pray that God aligns me back on my purpose and on my path, I pray that my ni**a didn’t really feel no way. And if he did, my ni**a I got my chin out. Take your best shot, I’ma take that sh*t on the chin. Boy, do what you do. All good.”

Nilichoelewa mimi,

Cole alijihisi kutokuwa sawa ‘spiritually’ baada ya ku downgrade ukubwa na mafanikio ya Dot kwenye game ("blessed to even stand beside...chase their greatness"). Na anakiri kwamba 7 Minute Drill ("the lamest, goofiest sh*t") haiakisi hisia zake za kweli bali ni matokeo ya msukumo wa nje kutoka kwa mashabiki ambao wao wanapenda hizi bifu marapa waparurane kama hivi wafanyavyo Drake na Kendrick Lamar hadi kusemeana mambo mazito na ya ajabu (“the world want to see blood").

Anakiri kwamba amekosea na anajisikia vibaya
("I moved in a way that, spiritually, I feel bad") na yupo tayari kuona au Kendrick akiijibu 7 Minute Drill
("my ni**a I got my chin out. Take your best shot").

Ni sehemu gani nyie wenzangu mmeona kuwa amemuogopa Kenny (zaidi ya kumheshimu)?! Au ndo tulishakubaliana kwamba Hiphop ni kusema tu mtu mwingine hawezi kuchana kukuliko na humheshimu? Hivi inahitaji digrii kuelewa kwamba
J COLE'S APOLOGY FOCUSES ON HIS REGRET and NOT HIS RAPPING ABILITY?

Tofauti na hao marapa wenu wanachofanya, J.Cole ameonesha kwamba anaweza kuviweka tofauti Diss track na heshima aliyonayo kwa kipaji halisi cha Kendrick Lamar! Na zaidi ametuonesha kwamba pressure ya rap beef (kutoka kwa media, mashabiki/internet) vilimfanya atake kutoka kwenye njia aloichagua.

Wote Cole na Kendrick ni wachanaji wakali, kuhusu nani ni zaidi ya mwenzie hilo ni personal preference…binafsi naenda na Cole. Yeye kujutia diss track yake na hata kuifuta kwenye streaming platforms haimaanishi kwamba ndo angeshindwa kungetokea beef, tuelewe kuwa jamaa hakuumbwa hivyo.

Nikim quote Nipsey Hussle, ambae nae inawezekana alimquote mtu, alisema “Would you rather be at peace with the world and at war with yourself? Or at war with the world and at peace with yourself?". Cole amechagua amani yake binafsi, ingawaje sote tunajua kuwa in terms of rap skills, bato ya Kendrick Lamar na J.Cole isingekuwa open kama ilivyo ya Kendrick Lamar na Drake.

J. Cole prioritized staying true to himself over industry expectations.
 
Cole is a "nice guy". Alitamani kushindana na K dot na Drake, ila mwisho siku alijua, ukishaweka miguu yako miwili kwenye hii safari, there is no going back!

Na mwisho, alijua hakutakua na mshindi zaidi ya kuvuananguo tu na kuendeleza chuki. Mambo mengi personal yamewekwa hadharani, alafu bado hakuna aliekubali kushindwa. Drake amebaki na mashabiki zake, na Kdot amebaki na mashabiki zake.

Kwangu mimi Drake Vs K dot, Cole is the winner!
 
Kweli kabisa
 
Mimi nitakupinga mpaka kesho ndugu yangu, nitakupinga mpaka vidole viote sugu kwa kutype.
Labda kama haumfuatilii mjomba living legendary, rap genius mwenyewe jcole. Ila kwa loyal fans wake kama mimi, Cole hastahili kabiiiiisa kuingia into a rap battle au kutoleana diss tracks n hao marapa 2. Kwa ufupi, ni kujivunjia n kutuvunjia heshima mashabiki zake kumfananisha Cole n mtu kama Lamar. Ukitaka kubisha, naomba usikilize icho kipande cha mwimbo wa shukran na utauelewa uwezo wa Cole.
Huyo mwamba ni next level, hauhitaji kutumia nguvu nyiiiingi kumuelewa. Nyimbo zake hatumii misemo n mavocabularies bali simple understandable language. Juu ya yote, ujumbe ndani ya nyimbo zake ndio shiiiiida na hii ndio tofauti yao. Kwa wale wanaopenda mabeats mazito yanayogonga mithili yaamapiano, ambayo ni lazima uumize kichwa kuelewa ujumbe, basi Lamar ndio mtu wao. Ila tukirudi kwenye ujumbe unaobebwa kimkakati kwenye nyimbo, hakuna anayestahiki kushika hata namba 2 baada ya Cole kati ya hao wa2.
So ningependa kukukumbusha tu kuwa Cole hakuogopa kuwa madogo wangempoteza kwenye game, hakutaka madogo waendelee kutembelea kivuli chake kwa kutrend kwa kubishana nae. Kwanza Cole sio mtu wa Kiki. Mwisho, inaingia akilini kweli kumfananisha mondi n marioo??? Au dully na baraka the Prince??? Au fid q na young dee??? Long live Cole, ningekuwa n uwezo ningetoa at least miaka 5nimpe cole ili aendelee kuishi maisha marefu zaidi. Huyo mwamba alimfanya hadi Jay z shushe ego yake n kuvinja sheria alizoziweka ili kuweza kufanya nae kazi. Tafadhali toeni wazi la kumpambanisha Cole n vitu vya kipumbavupumbavu
 
Attachments

  • J Cole - Note to Self [2014 Forest Hills Drive].m4a
    13.3 MB · Views: 2

Kaka unajibu heading, ungesoma content usingesema "Mimi nitakupinga mpaka kesho ndugu yangu, nitakupinga mpaka vidole viote sugu kwa kutype..." Mana hujanipinga bali umeniunga mkono
 
Nimekupata, nilisoma intro +2 extra paragraphs. Hakuna kama cole✋🤚
Toa pumba zako hapa!
Hakuna kama Cole!?
Huyo Cole amemzidi nini Kendrick!?
Hakuna kama Cole, huyo Cole hata kwenye kumi bora ya rappers wakali wa muda wote hayumo!

Namkubali sana Cole, ila ukianza kuleta habari za kumpamba hivyo siwezi kukubaliana na wewe!
 
Yani kwamba J cole aliomba msamaha akisema “Kendrick Lamar nisamehe bwana najua siwezi kubato nawewe uwezo wangu mdogo kukuliko” au maneno mengine lakini yenye maana sawa na hayo?
Mkongwe, sio mimi naamini hivyo, rap community ndo inaamini hivyo. Siku Cole anaomba msamaha rap community iliona amefanya jambo la kijinga sana, kuandika diss mpaka inawafikia mashabiki ni mchakato mrefu, sasa diss track imeshawafikia mashabiki kabla uliyemdiss hajakujibu wewe umekimbilia kuomba msamaha, mzee kwenye hip hop community that’s a pussy move, haijalishi ana excuse gani.
Mzee mimi sio shabiki wa Kendrick, nina albamu karibia zote za J.Cole pia nina albamu karibia zote za Kendrick, hawa wawili wote nawasikiliza na ninawaelewa sana!
 
Cole is a "nice guy". Alitamani kushindana na K dot na Drake, ila mwisho siku alijua, ukishaweka miguu yako miwili kwenye hii safari, there is no going back!

Na mwisho, alijua hakutakua na mshindi zaidi ya kuvuananguo tu na kuendeleza chuki. Mambo mengi personal yamewekwa hadharani, alafu bado hakuna aliekubali kushindwa. Drake amebaki na mashabiki zake, na Kdot amebaki na mashabiki zake.

Kwangu mimi Drake Vs K dot, Cole is the winner!
I say j cole is a smart guy, unajua hiz conflct zimekuwa designed kuwapa raha mashabiki but si kuwafaidisha wasanii. I say cole is smart for choosing his battles, ambazo zinge chafua his image
 
Mimi nitakupinga mpaka kesho ndugu yangu, nitakupinga mpaka vidole viote sugu kwa kutype.
Labda kama haumfuatilii mjomba living legendary, rap genius mwenyewe jcole. Ila kwa loyal fans wake kama mimi, Cole hastahili kabiiiiisa kuingia into a rap battle au kutoleana diss tracks n hao marapa 2. Kwa ufupi, ni kujivunjia n kutuvunjia heshima mashabiki zake kumfananisha Cole n mtu kama Lamar. Ukitaka kubisha, naomba usikilize icho kipande cha mwimbo wa shukran na utauelewa uwezo wa Cole.
Huyo mwamba ni next level, hauhitaji kutumia nguvu nyiiiingi kumuelewa. Nyimbo zake hatumii misemo n mavocabularies bali simple understandable language. Juu ya yote, ujumbe ndani ya nyimbo zake ndio shiiiiida na hii ndio tofauti yao. Kwa wale wanaopenda mabeats mazito yanayogonga mithili yaamapiano, ambayo ni lazima uumize kichwa kuelewa ujumbe, basi Lamar ndio mtu wao. Ila tukirudi kwenye ujumbe unaobebwa kimkakati kwenye nyimbo, hakuna anayestahiki kushika hata namba 2 baada ya Cole kati ya hao wa2.
So ningependa kukukumbusha tu kuwa Cole hakuogopa kuwa madogo wangempoteza kwenye game, hakutaka madogo waendelee kutembelea kivuli chake kwa kutrend kwa kubishana nae. Kwanza Cole sio mtu wa Kiki. Mwisho, inaingia akilini kweli kumfananisha mondi n marioo??? Au dully na baraka the Prince??? Au fid q na young dee??? Long live Cole, ningekuwa n uwezo ningetoa at least miaka 5nimpe cole ili aendelee kuishi maisha marefu zaidi. Huyo mwamba alimfanya hadi Jay z shushe ego yake n kuvinja sheria alizoziweka ili kuweza kufanya nae kazi. Tafadhali toeni wazi la kumpambanisha Cole n vitu vya kipumbavupumbavu
Drake ni GOAT😭😭😭😭
 
K dot sometime anakua rapcha mmarekani
Nini wewe!?
Nyie vijana mna matatizo, Kdot anakua kama Rapcha kwenye upande gani, kusokota nywele au kitu gani!?
Umenikera sana mkongwe, tena bahati mbaya nimeikuta hii hoja yako baada ya kutoka kuisikiliza SING ABOUT ME, IM DYING OF THIRST

Kula kibao hicho!

View: https://m.youtube.com/watch?v=75wmW7xjyog&list=OLAK5uy_mhYMgh1v0LpLuS0FqC693tfVkyVZK9WSQ&index=10&pp=8AUB

Halafu rudi tena hapa uniambie kuna mfanano upi kati ya Kdot na Rapcha, ukiacha kusokota nywele na jinsia.
 
Haya yote yanakuja baada ya waliyemtarajia kashindwa!

Walijua Kendrick atashindwa! Wanaucheki ubao wanaona Drake yupo chali.

Hapa wanatafuta tu milango ya kutokea na kuburudisha nafsi zao.

Kwa anayeujua mziki, kwa anayejua hip hop hawezi kubisha uwezo wa Kendrick.

Hata kwa wao wenyewe mziki ulipotoka wasanii wengi walikuwa wakimtahadharisha Drake ya kuwa battle aliyoichagua ipo juu ya uwezo wake. Lakini hatukuona wengi wao wakimwambia hayo maneno Kendrick kuhusu Drake. Jawabu lipo wazi! Wanautambua uwezo wa King Kendrick.

Hao wasikuumize kichwa ndugu yangu George. Haya yote yanakuja baada ya waliyemtarajia kashindwa.
 
Back
Top Bottom