ITV mbona mnafanya upendeleo kwa CCM?

ITV mbona mnafanya upendeleo kwa CCM?

Bavicha ni kulia lia subiri tarehe 27 ndio mtalia na kusaga meno....
 
Mhh ama.kweli mfa maji haishi kutapatapa JUZ TU MLISEMA ITV NDIO INATOA TAARIFA ZA UKWELI LEO HII TENA MNASEMA ETI HAIFAI KWELI MMEISHIWA SERA #HAPAKAZITU
 
Uchaguzi wa mwaka huu sijuwi itakuwaje.Jana mtu kaanzisha uzi hapa analalamika itv inapendelea Chadema leo mtu kaanzisha ccm inapendelewa.dawa kila Chama kianzishe kituo chake.
 
Wafuasi wa CHAMA CHA MAKAPI hawajielew kabisa,hawaushi kulialia
 
ITV wameipata hii wameona acha iwe mbwela mbwela tu.

Kuna mpango wa Mwenyekiti wa Chadema Mh.Freeman Mbowe wa kulipwa mamilioni ya fedha ili Viongozi wa Chadema waache kumsema Mr. Monduli kuwa ni fisadi.

Mh.Zitto Kabwe anajitahidi kwa kila hali kuzuia mpango huo

Na Mwandishi wetu | Gazeti la Sauti Huru

Mmoja kati ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi(jina tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya siri na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Freeman Mbowe ili kuingia ubia na chama hicho.

Inaelezwa kuwa ,lengo la kigogo huyo ni kukiziba mdomo chama hicho kisimrushie makombora ya ufisadi kama walivyowahi kumrushia siku za nyuma.

Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa gazeti hili kwa muda mrefu sasa umebaini kuwa kigogo huyo wa CCM amekuwa na mawasiliano ya siri na ya karibu na Mbowe huku vikao vingi vikifanyika ndani ya hoteli moja ya kitalii iliyopo jijini Arusha (jina tunalo)

Imebainika kuwa ndoa hiyo ya siri ni ya wanasiasa hao wawili,lakini ikilenga uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo kigogo huyo wa CCM amemuahidi Mbowe kwamba wataunda "serikali ya umoja wa kitaifa" endapo Mbowe atasaidia kuacha kumuandama kwa tuhuma za ufisadi na kuwadhibiti viongozi wengine wa chama chake, kutofanya hivyo kwenye maandamano na mikutano yao ya hadhara, pamoja na kwenye mahojiano na vyombo vya habari.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa tayari kigogo huyo amempa mwenyekiti huyo wa CHADEMA kiasi kikubwa cha fedha ili chama hicho kinapoendelea na kampeni yake ya bomoa-bomoa mafisadi yeye asiguswe kabisa, kama hatua ya kumfikisha ndoto yake ya kutaka chama tawala kumteua kuwa mgombea wa nafasi ya urais.

Chanzo chetu cha uhakika kikiongea na Sauti Huru kwa sharti la kufichwa jina lake kimedai " huu mpango unafanywa kwa siri kubwa na ninajua hata mhusika (anamtaja) akijua habari hii imetoka atafadhaika sana"


Habari zaidi zinadai kwamba kigogo huyo amefikia hatua hiyo baada ya kusoma alama za nyakati na kuona kwamba uwezekano wa mwenyekiti wa chama chake kumuunga mkono ni mdogo, hivyo hatoweza kupenya katika kinyang'anyiro cha uraisi 2015.

" Huyu bwana amesoma alama za nyakati ,ameona kabisa uwezekano wa kuungwa mkono na mwenyekiti wake(wa CCM) ni mdogo sana hivyo ni lazima atafute njia nyingine hata kama njia hiyo itakuwa na madhara kwa chama chake", kilieleza chanzo hicho na kufafanua;

"Si kwamba hajui mwenyekiti atalalia wapi, anajua lakini yuko tayari hata kukisaliti chama ili wote wakose,hivi ninavyoongea nanyi watu hawa wana mawasiliano ya kila mara juu ya suala hili ila Mbowe kaweka ngumu kuwa lazima waandikishiane ajue kabisa endapo (kigogo huyo atafanikiwa kuingia madarakani basi wataunda government of unity(serikali ya umoja wa kitaifa)".

...Aidha imefafanuliwa kwamba habari hizi zimeweza kumgusa hata Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, lakini kwa namna ya pekee Zitto ameweza kudhoofisha mkakati huo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni 'unafiki kwa Mbowe'

"Mtakumbuka siku za hivi karibuni Zitto alishutumiwa na chama chake kwa madai ya kuwa na uhusiano wa mashaka na Idara ya Usalama wa Taifa. Chadema wamekuwa wakidai kwamba Zitto anatoa siri za chama chao nje na hata kumuundia kamati ya wazee kumshauri?" alihoji.

Aliendelea:" Kilichotokea katika kamati hiyo siku walipokutana na Zitto ilikuwa tofauti kabisa, Zitto akawabadilishia mada pale alipowaambia wazee,'jamani ugomvi wangu na Mbowe ni pesa za chama, anatumia chama hiki hiki kupata fedha toka nje ya nchi na ndani ya nchi, lakini ninapojaribu kumkosoa kuwa tabia hiyo si nzuri kwa mwenyekiti wa chama ananijia juu,nyie mnajua kuwa amepokea fedha mamilioni kutoka kwa(anamtaja kigogo huyo) kwa ajili ya kutunyamazisha tusipige kelele za ufisadi dhidi yake?' "

"Hivi hamjui tayari anafanya mazungumzo na mtu wa CCM kwa ajili ya power sharing ya mwaka 2015?"

Kwa mujibu wa habari hiyo ni kwamba kigogo huyo atafanya kila liwezekanalo CCM imteue kuwa mgombea wa nafasi ya uraisi; lakini anajua hilo litawezekana endapo kelele za ufisadi dhidi yake zitamalizika.

"Huyu mtu ni mjanja sana na kwa sasa ana nguvu na mtandao mkubwa ndani ya CCM unaoweza kumfanya ateuliwe na chama kuwa mgombea, si hilo tu anajaribu hata kutafuta nguvu nje ya nchi ili endapo akikataliwa aweze kuwa na cha kuieleza jumuiya za kimataifa,"

"Na kwa hatua aliyofikia ni kwamba endapo hatoteuliwa hasa kutokana na ufisadi wake,yuko tayari hata chama chake kipoteze nafasi ya uraisi kitu ambacho kinaonyesha kuwa hana sifa za kiuongozi isipokuwa ni tamaa ya utawala."

ITV wameipata hii wameona in ujinga wacha iwe mbwela

Source: Gazeti la Sauti Huru

My Take:
Wale viongozi wa Chadema na wakereketwa waliopo humu JF watuthibitishie hii habari kama ni kweli.
 
Kituo cha ITV leo kimeushangaza umma wa watazamaji wake kwa kitendo cha kutangaza habari za chama kimoja wakati matukio ya vyama vyote yanafanana. Tunapenda kuuambia uongozi wa ITV utambue kuwa vyama vyote vina haki ya kutangazwa habari zake ili Watanzania waweze kuzipata. Ni imani yetu kituo hicho kitatuomba radhi watazamaji wake ambao tulitegemea kupata habari hizo kupitia ITV.


Relax mkuu.
Usipanic.
Mbona jambo dogo sana hili?
Numbers don't lie.
Wacha namba ziongee. Tunaanza J2 hii.
Hamna hata haja ya kuwalipa waje kuchukua matukio.
Watatutafuta wenyewe na watarusha habari pasipo kuwapigia magoti.
 
hata mimi jana nilitia huruma sana nilikodolea tv kwa kudhani ningepata habari zetu kama kawaida mpaka nikadhani nimekosea channel lakini ni ITV how jamani...sikulala vizuri kusema ukweli.


....kumbe unakiri kuwa ni kawaida yake hiko kituo kukupatieni habari zenu. halafu nyie mibavicha mnakuwa kama ma**** yaani kazi yenu ni kulalamikalalamika tuuu kwakila jambo!!!! mi ni mfuatiliaji mzuri wa kituo hiko cha itv, hususani tangu pilika hizi za uchaguzi zianze. kama tutaamua kuwa wakweli, itv imekuwa na upendeleo wa wazi kwa ukawa tangu ilipopita ile trh 12 ambapo watu kadhaa walikatwa......takribani wiki nzima fulani hivi, habari ilikuwa ni kuhamia chadema kwa watu fulani hv kutoka ccm, mara maandamano ya wanachama wa ccm eneo fulani hv kupinga uchakachuaji ktk uchaguzi, mara kupigwa katibu wa ccm eneo fulani n.k. habari zilikuwa ni za ubaya ubaya ubaya kwa upande wa ccm na nzuri nzuri nzui kwa upande wa ukawa. nikiwa kama mtu ninayeipinga ukawa kwa sala zote, sikuwahi kulalamikia wala kuacha kuangalia kituo hiko. sasa mbona nyie mnakuwa kama wote ni mademu watupu....au kama jamaa zangu wale walionenea zaidi maeneo ya pwani ambao kulalamika kwao imekuwa kama ibada.......badilikeni watoto wa kiume , kwani tabia hiyo ikiendelea mtatuletea akina obama huu kuja kuoa kaka zetu........
 
Back
Top Bottom