ITV mbona mnafanya upendeleo kwa CCM?

ITV mbona mnafanya upendeleo kwa CCM?

yanga bwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2015
Posts
300
Reaction score
47
Kituo cha ITV leo kimeushangaza umma wa watazamaji wake kwa kitendo cha kutangaza habari za chama kimoja wakati matukio ya vyama vyote yanafanana. Tunapenda kuuambia uongozi wa ITV utambue kuwa vyama vyote vina haki ya kutangazwa habari zake ili Watanzania waweze kuzipata. Ni imani yetu kituo hicho kitatuomba radhi watazamaji wake ambao tulitegemea kupata habari hizo kupitia ITV.
 
Teh Teh UKAWA mmeanza kulia lia eeeh..
 
Sisi huku tuliko dodoma tumeshangazwa sana na itv,hata habari ya jimbo la mtama nayo imewashinda,wakati kwenye mtandao wao ipo.
 
Kwani nyie yenu mmemtisha Mzee Wa watu kuwa mtamuua
 
Dah Itv nyie ndo kimbilio letu tv ya taifa ni nyie vipi tena kulikon? Hatutak mtupendelee bt kuwen fair bas dah
 
Wamepewa maelekezo au ni kujikomba kwa chama tawala.huoni waandishi wengi waliokuwa nacho bega kwa bega walizawadiwa ukuu wa wilaya.uandishi maslahi.chezea tumbo weye!!!!!
 
ITV ni msumeno..unakata pande zote! Kwani habari za chama gani hazitangazwi ITV? Waambie wafanye yenye tija kwa umma nina uhakika hawataachwa kutangaza...na wengine pia wataendelea kupata fursa ya kutangazwa kama unaowataka wewe!
 
Hata kama sina chama... kwa hili jana na mimi limenishangaza, dkk 15 zooote kutangaza Magufur kupiga sahih tu na wakat huo huo Lowasa nae alikwenda kupiga sahh siku hiyo hiyo..

Shame on you ITV...!!! Kama kazi yenu ni kuwahabarisha Watz, wahabarishen bila kuwa na upande
 
Hata Mimi Wameniboa Sana. Msiwaogope CCM, Watakuwa Wapinzani Soon. Tunawaomba Nyeupe ibaki Nyeupe,na Nyeusi

Ibaki Nyeusi Msifiche Kitu Hata Kama Ni UKAWA/CCM. Haiwezekani Rais Wetu Eddo Lowassa Aende Kusaini Form Mahakamani

Mkashindwa Kuliona Hilo Na Badala yake Mkamwona Dr. Magufuli tu na MaCCM wenzake..
 
Hata Mimi Wameniboa Sana. Msiwaogope CCM, Watakuwa Wapinzani Soon. Tunawaomba Nyeupe ibaki Nyeupe,na Nyeusi

Ibaki Nyeusi Msifiche Kitu Hata Kama Ni UKAWA/CCM. Haiwezekani Rais Wetu Eddo Lowassa Aende Kusaini Form Mahakamani

Mkashindwa Kuliona Hilo Na Badala yake Mkamwona Dr. Magufuli tu na MaCCM wenzake..

İTV ni tv ya taifa!
 
Kwa kweli kitendo hicho kinashusha hadhi thamani ya vyombo vya habari kama ITV, kuna baadhi ya vyombo kama TV1 au Chanel 10, hawa Jamaa huwa ni waoga hatari kuonyesha habari za serikali ijayo ya UKAWA. Watabadilika tu muda ukifika maana UKAWA ni brand haihitaji Promo!!
 
Mnatafuta UBAYA bure na vyombo vya watu,hawa wamepigwa marufuku na wasipofanya walichoambiwa watafutiwa LESENI zao???

Ulimsikia jana Ruge akijiuma uma kujitetea? Kinachofanyika sasa ni kuua UHURU wa habari. Jamani, kama tunataka tufungue TV za vyama vyetu ndivyo havitakuwa na kufungwa au kupewa maagizo toka juu.
 
hata mimi jana nilitia huruma sana nilikodolea tv kwa kudhani ningepata habari zetu kama kawaida mpaka nikadhani nimekosea channel lakini ni ITV how jamani...sikulala vizuri kusema ukweli.
 
Kwa jana ITV walinikwaza. Na baada ya tukio lile jn nilizima Tv & sikuendelea kuangalia hbr zingine nikasubiria Bbc na VoA kwa akina Shaka Sally. Pia Channel 10, ile habari ya kusaini hati ya mahakama walitumia dakika zote kumwonyesha mgombea wa Ccm, picha ya Lowasa ilipoingia tu wakakata ... Tutawasusia na wao, kwa maana hatuna namna nyingine. Tumaini letu linabaki mitandao, na magazeti ...!
 
Back
Top Bottom