Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
Pamoja na kutambua umuhimu wa kupunguza kasi ya ongezeko la watu, lakini bado jitihada hazijafanyika za kuhakikisha kwamba kiwango cha uzazi nchini kinapungua ili kuendana na mipango ya maendeleo ya kukuza uchumi na kuondoa umaskini.
Kutokana na changamoto hiyo, kuna haya ya Serikali kutunga Sera ya kila kaya kuwa na watoto wawili ili kudhibiti ongezeko lililopo sasa.
Katika kufikia dira ya kuwa na uchumi wa kati, Tanzania inapaswa kuangalia mfano wa nchi nyingine zinazoendelea hususan ‘Miamba ya Maendeleo ya Asia’ kama Thailand, Malaysia, Korea ya Kusini, Taiwan na Indonesia ambazo zimeendelea kwa kasi tangu miaka ya 1960.
Zaidi, soma hapa => Itungwe Sera ya ‘watoto wawili kwa kila kaya’! | Fikra Pevu