Its a movement to reclaim our country, our values. Its not a mere campaign...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Its a movement to reclaim our country, our values. Its not a mere campaign...!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by jaxonwaziri, Sep 8, 2010.

 1. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Watanzania tumeshuhudia mbinu chafu za kila namna za kuharibu uwezo wa watanzania kutathmini na kufanya uamuzi sahihi juu ya kiongozi anayefaa kuongoza taifa hili ifikapo October 31.
  Wametumia rushwa, wametumia kashfa juu ya maisha binafsi, wametoa hela ili magazeti yachapishwe na kugawiwa bure n.k
  Watanzania wenzangu, tuinuke kwa pamoja kuhamasishana kwamba hatuitaki CCM tena, maana kwa sasa huu ni muamko thabiti kudai nchi yetu, utu wetu kutoka mikononi mwa mafisadi hawa! Tumedhalilika vya kutosha, tumevumilia vya kutosha. Tushikamane, tuikomboe nchi yetu, tummpigie kampeni na mwishowe tumchague Dk Slaa kuwa rais wetu ifikapo October 2010.
  Ni kweli hatuna fedha za kutosha kuweka mabango kila pahala, lakini pia hata nyerere alipokuwa anaikomboa nchi hii wakati wa ukoloni, hakuweka mabango kila pahala! Watu walihamasishana, wakahamasika, wakafanya maamuzi magumu na thabiti.

  INUKA MTANZANIA, HATMA YA TAIFA LAKO IPO MOKONONI MWAKO LEO.....!
   
 2. s

  skeleton Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kabisa kwa mada hii nzuri. Ni kweli Watanzania tuzinduke. Tupingane na hii aina mpya ya ukoloni! Ukoloni huu ambao umeletwa na baadhi ya viongozi wa CCM.

  Kwa kweli inabidi kupata uhuru toka kwenye makucha ya CCM ambao wamevunja sheria kwa kupitia ufisadi, katiba mbovu, mikataba mibovu, ufujaju wa rasilimali za nchi hii, udikteta, wizi n.k. Wameitia nchi hii katika lindi la umasikini mkubwa na kuathiri wananchi wake kwa kiwango cha hali ya juu saana!

  Ukoloni huu una athari sana kama ulivyokuwa ukoloni wa zama za ukoloni na kama ulivyo ukoloni mambo leo. Mbaya zaidi wakoloni hao leo hii ni chama tawala cha CCM, wakoloni hao ni amongst sisi Watanzania wenyewe! It is so sad, humiliating and drastic and vigorous changes are needed rightaway by wiping away CCM, THE COLONIALIST from leadership! The solution is Dr Slaa!
   
 3. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  (1) Kwa nini wamiliki na waandishi wa magazeti wanashindwa kuona kwamba baada ya mika 50 ya kutawaliwa na watu walewale bila mafanikio inabidi kufanya mabadiliko ya msingi?

  (2) Kwa nini wako vijana wengi wa Usalama Wa Taifa ambao wanakubali kudanganywa siku zote kwamba tukibadilisha chama tawala kutakuwa na machafuko? Hawajui kikundi kimoja kuhodhi madaraka ndio sababu kubwa inayoleta vurugu nchi nyingi za Afrika? Hawaoni Kenya ilivyoneemeka baada ya kubadilisha chama tawala?

  (3) Kwa nini Jeshi la Polisi linafanya kazi kama idara ya CCM? Polisi hawaoni CCM imeshindwa kuinua hali ya jeshi lao na ya tafa kwa ujumla? Kama CCM imeshindwa hata kuwajengea nyumba za kulala katika kipindi cha miaka 50, miaka mingine 5 itasaidia nini? Wataandikia vipande vya mifuko ya sementi mpaka lini?

  (4) Kwa nini Kikwete hajatimiza ile ahadi yake ya kuwataja wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya? Kwa nini Makamba anakataa kuwaeleza Watanzania kama ni kweli aliwahi kufukuzwa kazi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi kwa kosa la kubaka? Anataka tumweleweje?

  (5) Kwanini CCM inataka kuendelea kututawala kwa nguvu? Hatutaki tena. Tumewavumilia vya kutosha. Ondokeni kwa amani.
   
 4. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Hakika huu ni mwaka wa ukombozi, tuamue kuwatokomeza mafisadi, wahuni, wevi, mabazazi, wadwanzi, wachafu hawa wa ccm!!!
   
Loading...