Ukiona mtu yuko kwenye ndoa miaka zaidi ya mitatu basi..
Itoshe tuu kusema ndoa inahitaji uvumilivu
Ndoa ikikosa uvumilivu ni kama vile mikono na miguu kwenye gari vishindwe kuelewana, mikono inazungusha stearing kukata kona na miguu inakanyaga mafuta.
Kwenye ndoa inabidi ujifanye mjinga ili kumuepuka mpumbafu..
Unatoka kazini umechelewa ukitafuta riziki mke anakuuliza kwann umechelewa akihisi ulikuwa na mwanamke mwingine..
Kwenye ndoa mume/mke anaweza kuwa na matumizi yasiyo ya lazima kipindi ambacho wewe unahitaji kubana matumizi au hauna hela..
Kwenye ndoa mke anaweza kukutaka umgegede wakati ambao anajua kabisa uko na stress na hata hisia hauna [emoji4][emoji4] nyie ndoa ni vichekesho..
Kwenye ndoa mnaweza mkagombana na mkasameheana na kesho mke/mme akarudia jambo lilelile.. Ndoa ni kuvumiliana..
Nishauri vijana ambao hamjaingia kwenye ndoa, hakikisha huyo mpenzi wako unampenda na umeridhika nae, usioe kwasasabu anatuliza nyege zako, usiolewe kwasababu ukiwa na shida ndogo ndogo anakusaidia.
Vyote vinapita na vina majira hivyo hakikisha vikipita na akabaki yeye basi utampenda..
Miaka 8 kwenye ndoa