Itikadi,Sera,Ilani za uchaguzi na Kampeni 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Itikadi,Sera,Ilani za uchaguzi na Kampeni 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Jan 29, 2010.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Baada ya kutafakari kwamba huu ni mwaka wa uchaguzi kwenye ka- Nchi ketu haka maskini sana ulimwenguni (wa mipango) nimeona haya mambo ni muhimu sana kuhusiana na uchaguzi huo. Itikadi, Sera, Ilani za uchaguzi na kampeni.

  • Itikadi za vyama vyetu zinajibainisha na kuweka tofauti kati ya chama na chama?
  • Itikadi ipi ni bora kufuatwa na nchi yetu kati ya hizi tatu maarufu zaidi duniani?
   • Ubepari
   • Ujamaa
   • Uliberali
  • Ndoa za jinsia moja ziruhusiwe?
  • Uraia wan chi mbili uruhusiwe?
  • Muungano wa Tanzania uweje?
  • Tuwe na sarafu moja kwa Afrika ya Mashariki?
  • Sera za Tanzania kuhusu Mashariki ya kati ziweje na ziegemee upande upi, wa Waarabu au wa Waisraeli?
  • Tubadili mfumo wetu wa Elimu kutoka 7 – 4 – 2 – Chuo kikuu au tuache mambo kama yalivyo?
  • Lugha gani itumike katika kufundishia elimu kwenye mashule yetu na vyuo?
  • Sera yetu ya kilimo iweje?
  • Siasa iendelee kukatazwa kwenye taasisi za elimu au iruhusiwe?
  • Ilani za uchaguzi ziwe za wagombea binafsi au ziwe zinatokana na vyama vyao wanavyotoka?
  • vyama Vingine vina ubavu wa kushindana na CCM kwenye kampeni?
  Orodha ni ndefu…….

  Hapa hoja yangu kuu ni kwamba, sisi kama watanzania ndiyo tunapaswa kwa wakati huu kuamua mustakabali wa nchi yetu badala ya kusubiri mpaka baada ya uchaguzi ndiyo tuanze kulalama na kulialia kama watoto wadogo.
   
Loading...