UKWELIYAKINIFU
Member
- Oct 6, 2020
- 27
- 50
Wataalamu wawili wa masuala ya uongozi, Profesa Ronald Raggio na Dkt. Sherylle Tan wa chuo cha Claremont McKenna nchini Marekani, walipata kuhariri kitabu kiitwacho “Leader Interpersonal and Influence Skills: The soft skills of leadership”, wakielezea stadi anazopaswa kuwa nazo kiongozi, hususan katika enzi hizi.
Katika kitabu hicho zinatajwa stadi za uongozi, zikiwemo zile ziitwazo ‘laini’, ambazo zinaweza kutumika kumfundisha kiongozi mtarajiwa na /au kupima umahiri wa kiongozi aliyeko katika nafasi fulani. Makala haya yanalenga kutumia stadi tajwa, kama frameworkya kusaidia kuuangazia ustadi wa kiuongozi aliouonesha Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kiongozi mkuu wa serikali ya awamu ya Tano nchini. Hivyo makala yanafanya tathmini ya uongozi wake, kwa kuangalia sifa zake zilivyothibitika.
Kwa upande mmoja, kiongozi anapaswa kuwa mahiri katika stadi zilizozoeleka ikiwa ni pamoja na kuwa na dira, kupanga mipango vizuri, kufanya maamuzi sahihi (hata yaliyo magumu), na kuandaa mikakati thabiti ya utekelezaji wa mipango mbalimbali. Kwa upande mwingine, kiongozi mahiri ana uwezo wa kuvutia wafuasi, kutoa motisha, kushawishi, kuhimiza utendaji, kutumia mawasiliano yenye tija, kuwa mbunifu, kutatua matatizo, kutoa mrejesho wa utendaji, na kuwajibika yeye mwenyewe.
Ama kwa hakika JPM ni kiongozi mwenye maono na dira iliyo wazi kabisa. Tangia alipofanya kampeni akiwa mgombea urais mwaka 2015, JPM alikuwa na dira ya wazi inayoonyesha ni wapi anakusudia kuipeleka Tanzania. Alitamka bayana kwamba anataka Tanzania iwe nchi ya viwanda, ili kujenga uchumi wa kati. Sio tu alitamka hayo, bali aliwafanya mawaziri na wasaidizi wake wakaiamini dira hii na wakaingia katika vitendo vya kuhakikisha nchi inafika huko.