ITAWEZEKANAJE?

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,878
Reaction score
4,562
Taifa litakuaje kiuchumi wakati vijana wa kiume wamekazana kutafuta dawa zakunenepesha uume na kuongeza hamu ya ngono badala yakuhangaika kutafuta changamoto mpya kupata fursa za kiuchumi zenye tija,litakuwaje kwa mfano.

Taifa ambalo vijana wakike wanawaza kunenepesha makalio ili wanaume wawatamani badala yakuonesha namna wanahaki yakudai usawa,litakuwaje?

Taifa ambalo kijana aliyepata division IV anakuwa mwalimu,inawezekanaje?

Taifa ambalo hata nunda anahaki kikatiba ya kugombea ubunge,itawezekanaje?

Taifa ambalo aliyepata division IV kidato cha 4 anapata Distinction chuo,itawezekanaje?

Taifa ambalo wanafamilia wanakutana kwenye vikao kujadili migogorontu badala ya mambo ya kuwezeshana kiuchumi,itawezekanaje?

Taifa ambalo siasa inaongozwa kwa kiki na sio miiko,itawezekanaje?

Taifa ambalo wasomi wanashindwa kuleta suluhisho la mambo madogo itawezekanaje?

Taifa ambalo mwanamke kuolewa imekuwa big deal,itawezekanaje?

Taifa ambalo mzazi anategemea amuozeshe bintiye ili Apate chochcote,itawezekanaje?

Taifa ambalo wazazi wanawaza binti yao aolewe na mwanaume mwenye pesa badala yakumtengenezea mfumo mwanawao awe na pesa,itawezekanaje?

Taifa ambalo kijana wa kiume anawaza akutane na mtoto wa kike wa kishua ili achomoke maisha itawezekanaje?

Taifa ambalo kijana akisha kuwa na degree anaona kamaliza itawezekanaje?

Taifa ambalo kijana anapoanza chuo tu anawaza kumiliki Alteza itawezekanaje?

Taifa ambalo kijana anamiliki vyeti vya taaluma pasipo Elimu ,itawezekanaje??

Taifa ambalo mtu anasoma miaka 16 halafu anawaza kuajiriwa tu,itawezekanaje??

Taifa ambalo vijana wameamua kufanya siasa za kinafiki ili wapate teuzi,itawezekanaje?

Taifa ambalo VIjana wanasoma ili hapo baadae waweze kupeleka mkono kinywani,itawezekanaje?

Bado naendelea kujiuliza itawezekanaje??

#theforgottengenius
 
ITAWEZEKANA TU KWENYE MSAFARA WA MAMBA NA KENGE WAPO.
 
Hivi unajua Sex Sells ?

Yaani Sex ni among the most paying business; In short I can argue kwamba all businesses at the core you might find sex involved.....
 
Kwa hiyo unadhani Nini kifanyike ili IWEZEKANE?
 
Hivi unajua Sex Sells ?

Yaani Sex ni among the most paying business; In short I can argue kwamba all businesses at the core you might find sex involved.....
Any person whose reproductive health is fit,can have a desire to sex,but never give it a credit that much,let not it drive you crazy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…