Itapendeza zaidi....................

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,669
Reaction score
33,691
Hello Jf,

Moja ya sababu ,watu wa scandnavia wanaishi muda mrefu ni pamoja na careful diet,,

I just think na sisi tukibdilisha eating habits zetu then tutaishi miaka mingi,

Kwa kuanzia, sio kweli mpaka ule vyakula vya mafuta kama kitimoto ndio unenepe,

Ugali,wali,chapati,maandazi hivi ni vyakula in excess vinanepesha,

Nimefikiria,life span yetu ni miaka 65,

Je tuki cut off carbohydrates/starch,tutaishi Zaidi??

Karibuni
 
Pamoja na kuwa tunakula carbohydrate kwa wingi lakini mazingira tunayoishi yana tufanya tu-burn energy kubwa kila siku.
1. Fikiria leo tarehe 14, mshahara umeshaanza kusomeka inabidi utembee asubuhi ili upande basi moja kwenda kazini.

2. Kijijini kule baada ya kula dona na maharage usiku, asubuhi wanawahi shamba kabla jua halijawa kali na wanarudi na kuni za kupikia.
 

you are right,but labda tungekuja na statistics za magonjwa ya moyo,kisukari etc yanayowapata watu,ingawa japokua wana burn calories sana??,

labda mazoezi pamoja na eating habits is the way forward kama tunataka kuishi maisha marefu.
 
you are right,but labda tungekuja na statistics za magonjwa ya moyo,kisukari etc yanayowapata watu,ingawa japokua wana burn calories sana??,

labda mazoezi pamoja na eating habits is the way forward kama tunataka kuishi maisha marefu.
Ni kweli idadi ya wagonjwa wa moyo na kisukari inaongezeka lakini pia ukumbuke kuna factors kama

Genetic, wengine wanarithi genes ambazo zako prone kwa magonjwa haya.

Life style, mtu ana kunywa bia au brandy ( pombe in general) kila siku baada ya kula sasa hizo calories zote zinakwenda wapi?

Age pia is another factor, metabolism ya over 60 si sawa na ya 25 years old.

Pamoja na hayo elimu ya afya ni muhimu.
 

nachotaka kujua je ,tukibadilisha diet na ku ommit carbohdrates,tutaishi muda mrefu????
 
nachotaka kujua je ,tukibadilisha diet na ku ommit carbohdrates,tutaishi muda mrefu????
Hatuwezi kuacha kabisa kula carbohydrates ndiyo ni shati ya mwili, ndiyo maana tuliambiwa balanced diet ni muhimu. Elimu izingatie excess consumption ya sukari ni hatari.

Kunywa maji zaidi badala ya soda
Ikiwezekana kuacha kutumia sukari kwenye chai kwani carbohydrate ya vyakula vikuu kama ugali au wali inatosha.
Kunywa pombe in moderation.
 

mnh,

mie nilikua na highlight jinsi culture yetu inavyotupeka kaburini early kwa ku consume much carbohydrates/starch....chapatti,ugali,wali............

balanced diet ni za wahenga,siku hizi sio balanced diet bali low carb diet..😀😀😀.

anayeandika hapa,ni kibonge cha kutupwa....😀😀😀
 
you are right,but labda tungekuja na statistics za magonjwa ya moyo,kisukari etc yanayowapata watu,ingawa japokua wana burn calories sana??,

labda mazoezi pamoja na eating habits is the way forward kama tunataka kuishi maisha marefu.
Uishi maisha marefu ili iweje?
Sema kuishi na afya njema, siyo kuishi maisha marefu.
Maisha marefu hayafai, yana changamoto nyingi sana ambazo usipotuliza kichwa hauwezi kuzielewa.
Nianze kwa kutoa mfano ufuatao kuweka sawa juu ya kwanini siyo vizuri kuishi maisha marefu kupitiliza "toleo lako".
Kama rika lako, yaani mliozaliwa muongo moja, wakaishi miaka 60-70 wote wakaisha, wewe kuishi miaka 20 zaidi mbele ili u-gain nini, kama siyo kuonekana kero tu?
Binadamu tuna nature moja yenye kufanana ya ajabu sana.
Kwa mfano rika lako wote wakiandikishwa shule, wewe ukabakizwa, lazima utajisikia vibaya.
Rika lako wote wakioa ama kuolewa wewe ukabakia, lazima itajisikia vibaya.
Rika lako wote wakijenga familia zao na miji yao na maendeleo yao mbalimbali, wewe ukawa bado umepanga, lazima utajisikia vibaya.
Rika lako wote wakifa kwa uzee, wewe ukabaki, pia utajisikia vibaya tu.
Binadamu tunazaliwa kwa matoleo. Toleo lako likiishapita kuna adha kubwa sana utakayopambana nayo. Utabaguliwa kwamba wewe ni zilipendwa na kila mchango wako utakaoutoa aidha kwa kutumia uzoefu wako, mchango wako huo utapokelewa kwa ajili ya kukuridhisha, lakini kiuhalisia utaonekana kuwa umepitwa na wakati na kupuuzwa.
Walimwengu wanapenda kizazi kipya na mambo mapya.
Wewe mwenyewe ni shahidi. Furaha gani unayoipata pindi unapomtazama mtoto mchanga na furaha gani unayoipata pindi unapomtazama kikongwe anayekaribia "kukata"?
Mitazamo hakika lazima iwe tofauti.
Tuongelee kuishi maisha ya afya, lakini si maisha marefu.
Maisha marefu maana yake ni kuishi kupitiliza life span ya "wananzengo".
 
Fanya calculations ya calories unazohitaji kwa siku, kula hizo na jitahidi njia ya kuunguza excess.
Kuna wakati nilifanya ya kula mlo mmoja kwa siku nilitaka kupendeza kwenye nguo nilifanikiwa lakini siyo nzuri kwa afya. Unatakiwa kula portion ndogo ndogo tatu kwa siku.
 
Nephew wangu aliniambia kheri aishi miaka 50 to the fullest kuliko 90 years of miserable life kuchagua cha kula😀
 

Kama unaishi kwa kufanya comparison na wenzio,basi kazi unayo,

yaani wenzio wakifa kwa uzee,wewe ukabaki utajiskia vibaya au utamshukuru Mungu kwa kukupa uhai????
 
nadhani lengo ni kuishi maisha marefu yenye afya tele/njema sio ilimradi kuishi maisha marefu tu.

umri mkubwa una changamoto zake nyingi.
 
Kama unaishi kwa kufanya comparison na wenzio,basi kazi unayo,

yaani wenzio wakifa kwa uzee,wewe ukabaki utajiskia vibaya au utamshukuru Mungu kwa kukupa uhai????
Rebecca huo ni mfumo wa kiulimwengu mama.
Tuanzie na mfano katika eneo dogo tu, spouse mliyeishi naye miaka nenda rudi, akifa huwa hakuna mbadala wa kuziba pengo. Ndiyo maana anayeachwa huwa naye hawaii kufa.
Vifo hivi huharakishwa na ombwe la upweke.
Nikija kwa rika, napo hivyohivyo. Wenziyo wote wakitangulia mbele za haki, ukaachwa peke yako, utakosa mtu wa kuliwazana naye ama kubadilishana mawazo, hautembelei wala hautembelewi, age inakutenga bila wewe kutaka, lazima ukumbwe na upweke.
Pigo letu kubwa wanadamu ni magonjwa, tunamuomba Mungu siku zote atuepushie magonjwa tuishi kwa afya njema na kifo chema.
Tunapojadili maisha tujadili afya njema na si maisha marefu.
Idadi ya miaka ni namba tu.
...'aliishi miaka mia lakini aliishafariki'... Yaani kufa ni lazima.
Sasa unakufakufaje, hiyo ndiyo changamoto ya maoni tunayovutana.
Ninajua hautokubaliana na mimi kwa sababu binadamu hatupendi na hatuzoei kifo. Tunataka tuishi maisha marefu, bila kujua hayo maisha marefu yana sura gani huko mwishoni, watu wanapoteza uwezo wa kufikiri, kuona kusikia, kutembea, nk nk. Hata hiyo faida ya kuishi kwingi baadaye hugeuka kuwa ni hasara.
 
Nilivyomuekewa Brenda ni kuwa, kama wote tukibadilisha life style na kula kiasi kidogo au kuacha kula kabisa wanga tutaongeza umri wa kuishi. Kwahiyo tutakuwa wengi wa miaka 110 mfano
 
Nilivyomuekewa Brenda ni kuwa, kama wote tukibadilisha life style na kula kiasi kidogo au kuacha kula kabisa wanga tutaongeza umri wa kuishi. Kwahiyo tutakuwa wengi wa miaka 110 mfano
Nimemuelewa vema.
Ma calories, ma carbohydrate yanavyosagwa na kuyeyushwa mwilini mwa mtu, inategemeana sana na shughuli za kila siku anazozifanya. Pia maumbile ya mtu ki-dna.
Tunashauriwa kufanya mazoezi ili kubalansi uyeyushaji wa mazagazaga hayo mwilini mwetu na siyo kuacha kuyatumia.
Elewa kwamba watu wengine wanakula chakula kwa ajili ya anasa na starehe, si kwa ajili ya kushiba, wanaita kujichana.
Sasa kumbadilisha mtu anayekula chakula kwa ajili ya faraja na starehe, ni ngumu sana kubadilika.
 
Vyuma vilivyokaza hivi kula mara tatu kwa siku kwa wengi ni starehe. Shost aliniambia amekwenda kwa dada yake amemkuta amepiga chakula amewapa watoto tu yeye anasubiri jioni. Chakula kulikuwa kidogo.
 
Mleta mada umejaribu kuangalia hali ya kipato kati ya watu wa Scandinavia na sisi? Uku kwetu tunakula ili tuishi wenzetu wanakula kutengeneza afya na siha njema.
 
Kuishi ni kuchagua.
Ila katika yote elimu juu ya hayo mambo inahitajika sana nyakati hizi.
 
ku cutt nawezekana ila wengine uwezo wao ni wa kupata hivyo vyakula sasa inakuwaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…