Itakuwaje Lowassa akiamua kurudi CCM?

Mwanaume haoti MCHANA! Ni fedheha sana kwa mwanaume halisi kuota ndoto za kipumbavu MCHANA kweupeeee! Unategemea huyo MTU wako atagombea na kuwa Rais wa Nchi hii tena? Thubutuuuuu! Uwe na akili japo kidogo!!
Najua tuko tofauti kifikira ila jaribu kujikita kwenye mada na mantiki yake kidogo
 
Myopic thinking.
 
Inawezekana ametumwa na Mzee kupima upepo ili "Akatwe mkia"!
 
Mkuu mimi na wewe ni mashahidi kungekua na demokrasia ndani ya chama Magu kwenye uenyekiti angeangukia pua
Kungekuwa na demokrasia ndani ya Chadema Lowasa asingepewa nafasi ya kugombea urais. Dr. Slaa asingedharaulika na kutukanwa na Chadema, maana yeye ndiye aliyeifanya Chadema iwe na kiki.
 
Huwezi amini; mimi sio mtabiri wala mganga wa kienyeji, natumia dalili zinaoonekana wazi kwa werevu wa mambo. muda mchache kabla ya mwaka 2020, ambao ni mwaka wa kinyang'anyiro cha uchaguzi itatokea kuhama kwa vigogo wakubwa wa siasa nchini na kuhamia chama tawala CCM, kama si kuhama basi lile kundi lillilohama...likiongozwa na mkubwa wao litarudi kundini mara baada ya mazungumzo ya muda mrefu na makubaliano baina ya marafiki wawili. Upande wa upinzani utakua na siasa za mtu mmoja mmoja, hawatafanya kazi kama timu tena, watavurugana na kila mtu atakwenda kutetea nafasi ya ubunge, hawatakua na presidential material, waliomuandaa atakua amewatupa mkono. Jamaa yule atarudishwa kuokoa jahazi upande wa pili kwa kuwa kinachoendelea kwenye nyumba yetu hatukukitarajia, tunapiga hatua za haraka RETROkurejea.... hapo kutatokea tafrani kamati kuu ya chama baada ya jamaa yule kutaka amalizie na jamaa yule aliyerejea kundini au aliyerejeshwa kutaka kuingia akasawazishe palipoharibika, hapa itakuwa balaa kubwa ila kwakua mtandao ni imara na wanakamati watakua wameisoma namba sana watafanya kila juhudi safari ya jamaa aliyeko mzigoni isite. FORGET ABOUT OPPOSITION TO LEAD THIS COUNTRY, EVEN 100 YRS I DON SEE IT....... TOROKA URUDI
 
Walah utabiri huu!! We ni nabii nani mzee jitambulishe
 
Ndoto za Alinacha kupiga teke kapu!
Huyo Magu wako ngoja akunyatie kama kesho hutakuwa Segerea!
Hizi ni ndoto za kichochezi. Nyambaf!
 
Chukua kioo ujitazame kama umeshanawa uso baada ya kushituka kutoka usingizini.
 
Mleta mada ameongea kweli kweli kweli tupuuuuu. Hongera sana kwa maono
 
Yaani ng'ombe aliyekatwa mkia apewe uongozi wa zizi? Acha masikhara wewe? Kama umetumwa kutest upepo, mwambie bado unavuma vibaya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…