Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
๐ญ Inawezekana ikawa Habari mbaya kwako wewe developers au mtumiaji wa Simu za Android ambaye unapenda ku install apps nje ya soko la play store.
๐ญ Kupitia tovuti ya Android developers blogs, Google wametangaza Sheria mpya kwa watumiaji wa vifaa vya Android ulimwenguni, Google Wana mpango wa kuzuia watu ku install apps toka nje ya soko la play store kupitia mfumo wa sideloading.
๐ Sideloading ni ule mfumo wa watu kuweza ku install apps Mbalimbali kwenye Simu za Android bila kupitia kutumia program ya Google play store hivyo unatumia Google searches (browser yoyote).
๐ญ Ikiwa wewe ni developers na kama app Yako haiko kwenye soko la play store inakupaswa Google wakutambue. Google hawataangalia app Yako inafanyaje kazi Bali itakupa google wakutambue ili kuweza kuruhusu app Yako kutumika kwenye vifaa vya Android.
๐ญ Lengo kubwa Google ni kuwalinda watumiaji wa vifaa vya Android dhidi ya apps hatarishi kwenye vifaa vyao ili kuwa salama, mfumo huo utaanza kufanya Kazi kuanzia Mwezi oktoba mwaka huu 2025 ila Mpaka kufikia mwaka 2026 na 2027 utaachiwa ulimwenguni kote.
#google #android #bongotech255