ISTILAHI ZA UHALIFU NA USALAMA

ISTILAHI ZA UHALIFU NA USALAMA

Joined
Oct 5, 2015
Posts
90
Reaction score
483
Techint/Technical Intelligence;

Katika istilahi za kiusalama neno Techint humaanisha intelijensia ya silaha na vifaa vingine vya kivita vinavyotumiwa na nchi zingine. Ili taifa moja liweze kujilinda vema ni lazima kuwe na utaratibu wa kufuatilia maendeleo ya teknolojia ya silaha katika nchi nyingine, na ikiwa kuna ugunduzi mpya wa teknolojia bora zaidi katika taifa lingine basi ni muhimu kutafuta namna ya kujilinda na silaha hizo mpya, ikibidi hata kwa kuiba teknolojia hiyo.

Mbinu ya Techint huenda mbali zaidi na kutaka kujua udhaifu wa teknolojia mpya, idadi ya vifaa vya kijeshi vinavyotumia teknolojia hiyo katika nchi husika pamoja na tafiti zinazoendelea. Ikiwa kuna ugumu wa ukusanyaji wa taarifa hizo, basi nchi moja inaweza kununua vifaa hivyo kutoka nchi nyingine na kuvifanyia uchunguzi ingawa biashara ya silaha baina ya mataifa hasimu ni suala adimu.

Wakati mwingine hutokea bahati kwa nchi moja kupata nafasi ya kumiliki silaha kali iliyotengenezwa katika nchi hasimu, mfano; Septemba 6, 1976 rubani wa jeshi la Sovieti/Urusi aliyeitwa Viktor Ivanovich Belenko alitoroka na ndege hatari ya Urusi aina ya MiG-25 (Foxbat) hadi mjini Hakodate, Japan. Wamarekani walimpatia rubani Belenko hifadhi, kisha wakaichambua mwanzo mwisho ndege hiyo ya MiG-25 ili kujifunza teknolojia iliyotumika kuiunda. Israeli nayo ilimtumia rubani Munir Redfa wa Iraq, aliyekubali kutoroka na ndege ya jeshi la Iraq aina ya MiG-21 iliyotengenezwa pia Urusi, na kuifikisha Israel.

Mafanikio ya operesheni hiyo ya mwaka 1966 iliyoitwa 'Operesheni Diamond' yalisaidia Marekani na Israel kujifunza zaidi teknolojia ya ndege za Urusi kwa kuichambua ndege hiyo, na hasa ilisaidia Israel wakati wa vita ya siku sita dhidi ya mataifa ya kiarabu (Six day War), mwaka 1967. Ndege za kundi la MiG zinatajwa kuwa ndege zilizotumika kwa wingi zaidi katika vita kuliko ndege zote za kivita duniani.

Nunua usome zaidi ndani ya kitabu cha ISTILAHI ZA UHALIFU NA USALAMA
Bei ni Tsh. 35,000/=
Kitabu kinapatikana popote Tanzania.

Piga simu;
0713933736
0745830775
0713606062
IMG_20200328_122708_946.jpeg
images%20(19).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom