Issa Bulilo mwenyekiti UVCCM Moshi Mjini anena

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
250
408
SIKU CHACHE ZIMESALIAKUELEKEA UZINDUZI WA KAMPENI

Ni #ISSA E J #BULILO
MKITI UVCCM MOSHI MJINI.

Nami naguswa kusema machache kuelekea Oktoba 28/2020

Tar20/8/2020 KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA ILIWATEUWA NA KUWATANGAZA WAGOMBEA UBUNGE WA MAJIMBO

NISEME KIDOGO JIMBO LANGU PENDWA LA MOSHI MJINI

Kamati kuu ilimteua na kumtangaza Ndg Priscus Tarimo kuwa mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini.

Ndg wanaCcm wenzangu na Vijana wenzangu waCcm waomba kura na kisemeo chema cha mazuri ya Chama na Mema yote yaliofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mwamba Imara Dkt. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI tunaowajibu na kazi kubwa kujibu hoja za wapinzani kwa kuyataja mazuri yote yaliyo tekelezwa

VIJANA tunaowajibu wa kutafsiri Faida ya Miundo mbinu iliyotengenezwa kwa faida ya Jamii zetu jamii ambazo baadhi ya watu hawaoni kilichofanywa na serikali ya Awamu ya Tano

Vijana kwa upande wa Jimbo tusimame imara kumsemea mgombea wetu wa Ubunge Ndg *Priscus* *Tarimo* tumsemee kwa jinsi Tumjuavyo kwani kashika Nafasi za Uongozi mbalimbali kwenye Chama na Serikali.

Vijana tukisaidie Chama kumsemea Mgombea wetu wa Ubunge kwani ni Nuru na Taa ya Wana Moshi kwa sasa Tuwaeleze wapiga kura Uzuri wa na uimara alionao mgombea wetu Uwezo wake wa kujenga Hoja na kuzisimamia

Vijana Tuwaambie wana Moshi kwamba Moshi mjini ya Kisasa inakwenda kuonekana pindi tu Priscus akishinda na kua Mbunge wa Moshi Mjini.

Vijana tuwaambie wapiga kura kwamba Priscus ndie atakae weza kusimama na kulinda Amani ya Moshi mjini pindi tu akiwa Mbunge

Vijana wenzangu twende tukawaambie wana Moshi kwamba Priscus ni msikivu mnyenyekevu na mweledi hivo hapana shaka tukimtuma atatuwakilisha vyema kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vijana tuwaambie wapiga kwamba Chama cha mapinduzi kimeimalika sana hvo mgombea ubunge wa Ccm ndie aliyefunzwa kwenye maadili na misingi ya Utu na huyu si Mwingine kwa Moshi hii isipo kua ni Priscus.

Vijana wenzangu niwaombeni wote tulijue na kulizingatia hili ili tuweze kushinda jimbo kirahisi ni vyema tuhakikishe tunashinda kata zote 21 za manispaa ya Moshi, hivyo tunapo omba kura za madiwani tuhakikishe tunaomba kura za Mbunge, raha ya CCM ni ushindi tu si vinginevyo.

Vijana wenzangu tuhakikishe tunaomba kura kwa kuwanadi na kuwasemea vizuri wagombea wetu wa Udiwani ili tukapate heshima ya kuiongoza Manispaa huku tukiwa na Mbunge anae tokana na CCM.

Niwakati sasa wa Kusema basi miaka 25 ya Upinzani imetosha Tumuamini Priscus kwa Heshima ya Chama cha Mapinduzi Moshi Mjini

MUHIMU tukutane site tukiomba kura Ushindi wa Ccm ni bora kuliko kitu chochote

ISSA E J BULILO
M/KITI UVCCM MOSHI MJINI

FB_IMG_1598254881354.jpg
 
CCM tqngu lini ikawa na jipya.
Kuna wimbo maarufu sana wa ccm isiusahau: ,"CCM ni ILE ILE"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom