Israeli

Hizi ni porojo tu kwa sababu wengine wanasema Wapalestina wanadai kipande cha mashariki mwa ardhi ya Jerusalem kuwa ni eneo lao wengine eneo zima la Israel mimi hata sielewi
 
Halikubaliki miongoni mwa Wapalestina ambao wana hofu kuwa hatua hiyo itawafanya wapoteze utambulisho wao na kufanywa watu wa daraja la pili nchini Israel
Hapa inabidi watuombe sisi watz ujuzi tulioutumia kati ya Tangnyika na Zanzibar
 
Sasa udini hapo umeingiaje mkuu kama Arab league ni umoja wa kidini kwanini iran na pakistan ambazo ni nchi zi kiislamu hazipo? Na Lebanon ambao ina wakristo wengi ipo? Waarabu sio race kuna nchi nyingi ambazo zamani hawakuitwa waarabu ila baada ya ku adapt lugha na utamaduni wa kiarabu ndo wakaanza kuitwa waarabu. Ndo mana mnachanganya na kusema waarabu wamevamia misri au Palestine kwasababu mnafkiri arabs ni 1 race. wamisri na wapalestina ni wale wale ila wame adapt utamaduni wa kiarabu yaani wamekuwa Arabized sio wamevamia. Google "arabization" kama mdau hapo juu alivokushauri utaelewa zaidi
 
sasa kwa akili yako kwanini Iran na Pakistan wasiwe waarabu then Wasomali wawe waarabu. Issue ni moja tu, Iran siyo member kwa vile haziivi na baba yenu Saudi Arabia. Na wawe wahindi wa Kipakistan wanajua usanii uliopo katika arab League ndo maana hawana mpango nao.
 
Iran na pakistan hazipo arab league kwasababu wao sio nchi za kiarabu. Simple. Wana lugha na tamaduni zao tofauti na waarabu sio kwasababu za kisiasa. Mbona qatar haziivi na saudi arabia lakini wapo arab league?
 
Iran na pakistan hazipo arab league kwasababu wao sio nchi za kiarabu. Simple. Wana lugha na tamaduni zao tofauti na waarabu sio kwasababu za kisiasa. Mbona qatar haziivi na saudi arabia lakini wapo arab league?
haziivi sasa hivi baada ya Qatar ku-allign na Iran kwa Maslahi ya kibiashara. Wasomali hawana tamaduni za kiirabu. Wana tamaduni zao kama wasomali full stop.
 
haziivi sasa hivi baada ya Qatar ku-allign na Iran kwa Maslahi ya kibiashara. Wasomali hawana tamaduni za kiirabu. Wana tamaduni zao kama wasomali full stop.
Hata Iran haziivi baada ya mapinduzi ya kiislamu. Kabla ya hapo hawakuwa na tatizo na saudi arabia na bado hawakujiunga arab league. Iraq ya saddam zilikua haziivi na saudia, UAE, kuwait lakini walikuwepo.
 
Hata Iran haziivi baada ya mapinduzi ya kiislamu. Kabla ya hapo hawakuwa na tatizo na saudi arabia na bado hawakujiunga arab league. Iraq ya saddam zilikua haziivi na saudia, UAE, kuwait lakini walikuwepo.
nyie watoto wa mama mdogo tunawajua kwa ubishi wenu. Tuachane nahii mada. nenda ka swali swala ya ijumaa.
 
nyie watoto wa mama mdogo tunawajua kwa ubishi wenu. Tuachane nahii mada. nenda ka swali swala ya ijumaa.
Mi sio mwislamu Mkuu afu wewe ndo ulio ingiza udini kwenye hii mada sio mimi. Soma post zako vizuri
 
mimi sina chuki nao. tatizo wewe una mihemko. Mimi nimeuliza maendeleo gani Mwafrika atayapata kutoka kwa Mwarabu. waarabu waliwahi kuutawala Mwambao wa Afrika ya Masharaiki kwa miaka mingi kuliko mgeni yeyote yule. Wametuachia maendeleo gani?
Hivi na sisi wa Bara tulio tawaliwa na Wazungu tuna maendeleo gani

1.Poverty. ?????
2.Illiteracy rate. ??????
3.Malnutrition. ??????
4.Diseases ?????
5.Childhood Pregnancy
6.Mauaji ya Albino
7.Unemployment level
8.Divorce rate
9.STD and HIV
10.Corruption

Kuna factors gani ambazo waweza tumia kulinganisha Bara na Pwani ?
Ili useme Wabara(wakristo/wazungu) wameendelea kuliko Wapwani(Waislam/Waarabu)
Ni ujinga mkubwa saana kwanza kuwabagua watu ktk makundi hayo hasa ktk suala la maendeleo
Hao watu weupe wote ni Colonialists hawakuja kumfaidisha mtu, dini ililetwa as a MERE COINCIDENCE
 
Asante kwa kuuchukua muda wangu kwani nimesoma article yote bila kuruja hata nukta. Ila kupitia andiko hili nimegundua yafuatayo:

Umeandika kwa ustadi mkuu sana historia halisi ya chimbuko la wayahudi na wakaazi wa eneo la Palestine/Israel hasa historia hiyo ya kale kabla ya 24 May 1948. Baada ya hapo historia hiyo umeifunga funga kwa mafungu na ujumla wake hasa namna Waisrael walibyiweza kupora zaidi maeneo baada ya kuanzishwa kwa taifa lao. Vita walivyoshinda Wayahudu/waisraeli umeziongelea juu juu tofauti na ulivyofanya kwa upande wa pili hasa kwa Waislam ambapo uliweza kutaja si tu miaka bali hata majemedali walioongoza vita na hata kuandikiana mikataba na hata kunukuu sehemu ya mikataba hiyo (Eg Omar Mkataba)

Uandishi pamoja kwamba umejitahidi sana kuwrka ulinganifu wa kuwa hupendelei ipande wowote ila kwa wasomaji makini wataona uchambuzi huu na hata masulisho unayodhani yatamaliza mgogoro yamelemea zaidi kwa Waislam/palelstine kuliko hao tunaowaita walowezi!

Lakini tatu ni namna ya ajabu ulivyokwepa kuelezea kiunaga ubaga juu ya umuhimu wa mji wa Jerusalemu kwa muono wa Mayahudi na pia Ukristo. Hujaelezea ni namna gani mathalani imani ya kikristo inavyoamini juu ya mahali ilipojengwa Al Aqsa zaidi umeiongelea kwa mtazamo wa historia ya kale ya wayahudi na si kwa zama za baada ya kuja Kristo!

Otherwise nikupongeze sana kwa andishi zuri. Ukipata nafasi tupe historia sahihi ya eneo hilo na watu wake kwa mlengo wa circular!
 
Mkuu umechambua vizuri kabisa yaani nimesoma kuanzia mwanzo hadi mwisho hadi nikatamani isiishe

Hongera
 
umeongea points sana
 
heheee " safi sana
 
Kuna siku nitaifanyia makala ya video na sauti.. acknowledgement lazima maana ndo cha muhimu kuheshimu kazi za watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…