Israel inaingia na kufanya itakayo ndani ya Iran

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Apr 21, 2015
1,488
3,146
Hawa watu kwa kweli huwezi shindana nao,hata ufanyeje,wana akili za hali ya juu sana katika kupanga operation zao.

======

Mnamo Novemba 2020, msafara uliokuwa umembeba Mohsen Fakhrizadeh, mwanasayansi mashuhuri zaidi wa nyuklia wa Iran, ulishambuliwa. Aliuawa kwa bunduki iliyoelekezwa kwa njia ya teknolojia.

Kufanya mauaji kwa mtindo kama huo wa ufasaha dhidi ya shabaha inayosonga bila majeruhi yoyote ya raia kunahitaji msaada wa ujasusi katika eneo hilo.

Baada ya mauaji hayo, waziri wa ujasusi wa Iran, Mahmoud Alavi, alidai kuwa miezi miwili kabla ya hilo, alivionya vikosi vya usalama kwamba kulikuwa na njama ya kumuua Bw Fakhrizadeh katika eneo ambalo alipigigwa risasi.

Bw Alavi alisema mtu aliyepanga mauaji hayo ni "mwanajeshi. Hatukuweza kutekeleza shughuli za kijasusi kwa wanajeshi".

Lakini kwa njia isiyo ya moja kwa moja alidokeza kuwa mhalifu huyo alikuwa mwanachama wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), kitengo cha kijeshi chenye wasomi zaidi wa Iran. Ikiwa ndivyo, mhalifu huyo huenda alikuwa cheo cha juu katika IRGC ili kuweza kufuta onyo na kutekeleza mpango kwa tarehe iliyowekwa, saa na eneo.

Mohsen Fakhrizadeh pia anajulikana kuwa mwanachama wa IRGC.

Vyanzo vya habari ndani ya gereza la Evin mjini Tehran, ambako wale wanaotuhumiwa kufanya ujasusi kwa nchi za nje wanashikiliwa, zimeiambia BBC kuwa kumekuwa na makamanda wa ngazi za juu wa IRGC wanaoshikiliwa humo.

Serikali ya Iran haitangazi majina na nyadhifa zao ili kuepusha kuchafua sifa ya Walinzi wa Mapinduzi.

Afisa wa zamani wa ujasusi wa Kikosi cha IRGC (anayeongoza operesheni nchi za ng'ambo) ameambia BBC kuwa mashirika ya kigeni yamekusanya ushahidi dhidi ya mabalozi kadhaa wa Iran na makamanda wa IRGC.

Alisema hii ni pamoja na taarifa kuhusu mahusiano na wanawake, ambayo alisema inaweza kutumika kuwachafua maofisa hao ili kuwalazimisha kushirikiana na majasusi wa kigeni.

Mwishoni mwa Januari 2018, usiku wa manane, wanaume kumi na wawili walivamia ghala katika wilaya ya viwandani kilomita 30 kutoka mji mkuu, Tehran.

Kulikuwa na kabati 32, lakini walijua ni zipi zilizoku na vifaa vya thamani zaidi. Katika muda wa chini ya saa saba, waliyeyusha kufuli za kabati 27 kati yazo, wakachukua nusu tani ya kumbukumbu za siri za nyuklia na kuondoka bila kupatikana. Ilikuwa ni moja ya wizi wa ujasiri zaidi katika historia ya Iran, lakini maafisa walinyamaza.

Miezi mitatu baadaye, hati zilizoibwa zilionekana umbali wa kilomita 2,000, huko Tel Aviv, Israeli.

Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa wakati huo wa Israel, alionyesha nyaraka zilizoibwa, akisema zilipatikana kupitia oparesheni ya Mossad. Maafisa wa Iran wakati huo waliziita nyaraka hizo kuwa za uwongo wakisema kuwa tukio kama hilo halijawahi kutokea.

In 2018, Israeli PM Benjamin Netanyahu unveiled what he claimed to be Iran's secret atomic archive

Katika siku yake ya mwisho madarakani, Agosti 2021, Rais wa Iran Hassan Rouhani alithibitisha kuwa Israel iliiba nyaraka za nyuklia za Iran na kuonyesha ushahidi huo kwa Rais wa Marekani Donald Trump.

Akiwasilisha nyaraka hizo kwenye mkutano maalum wa wanahabari ulioitishwa mnamo Aprili 2018, Bw Netanyahu aliangazia jukumu la Mohsen Fakhrizadeh katika kile alichosema kuwa mpango wa silaha za nyuklia ambao haujatangazwa. "Dkt Mohsen Fakhrizadeh kumbuka jina hilo," alisisitiza. Bw Fakhrizadeh aliuawa miaka miwili baadaye.

'Piga risasi, usiongee'
Katika miongo miwili iliyopita, idadi ya wanasayansi mashuhuri wa nyuklia wa Iran wameuawa.

Kumekuwa na hujuma nyingi katika vituo vya nyuklia na kijeshi vya Iran, lakini hadi sasa vikosi vya usalama vya Iran vimeshindwa kuwazuia au kuwakamata washambuliaji na wapanga njama.

Katika mwaka wa mwisho wa urais wa Mahmoud Ahmadinejad mnamo 2013, kulikuwa na uvumi kwamba makamanda wa IRGC, maafisa wa ujasusi na hata maofisa wa kidini walikamatwa kwa kufanya ujasusi kwa Mossad. Lakini madai hayo hayakuwahi kuthibitishwa rasmi.

Mmoja wa washtakiwa alikuwa afisa anayehusika na upelelezi dhidi ya Israel katika wizara ya kijasusi ya Iran. Mahakama ya Mapinduzi ya Irani ilimtia hatiani kimya kimya, ikamhukumu kifo, na ikamnyonga kisiri.

Ni mwaka jana tu, Bw Ahmadinejad alithibitisha kuwa Mossad walikuwa wamejipenyeza katika wizara yake ya upelelezi.

Israel haitoi maoni yoyote kuhusu shughuli za Mossad. Jenerali mstaafu wa Jeshi la Israel (IDF) na afisa wa zamani wa wizara ya ulinzi Amos Gilad aliambia BBC, hii ilikuwa kwa sababu nzuri.

"Ninapinga utangazaji wowote. Ikiwa unataka kupiga risasi, piga risasi, usiongee ... sifa ya Mossad ni kufanya shughuli za ajabu, zinazodaiwa kuwa za siri."

Leo, maafisa wa zamani wa Iran wana wasiwasi kwamba Mossad imefikia maafisa wa juu katika taasisi za usalama na kijasusi za Iran.

Ali Yunesi, waziri wa zamani wa ujasusi wa Iran na mshauri mkuu wa Rais Rouhani, alitoa onyo hili katika mahojiano: "Ushawishi wa Mossad katika maeneo mengi ya nchi ni mkubwa kiasi kwamba kila mwanachama katikaa uongozi wa Iran anapaswa kuwa na wasiwasi juu ya maisha yake.
 
Israel is over rated, nawanatumia propaganda nyingi kwaminisha watu kwamba technology yao ni sophiscated sana, Israel imeshindwa vita nyingi na inapigwa sana isipokua wegi hawalifahamu
Hii mada imeelezea yale ambayo Mossad imefanikiwa kuyafanya katika Iran. Hoja husika imeungwa mkono na wasemaji kutoka Iran yenyewe na ndani ya Israeli. Kama unataka kuleta habari ya upande wa pili wa hizi habari, kama upo,anzisha mada na tutachangia kadiri tuwezavyo.
 
Kwa hali hiyo basi ile ndoto ya Iran kwamba ipo siku watakuja kumiliki silaha za nyuklia itabaki kuwa ndoto hivyo hivyo milele.

Kama watapiga hatua ya kukaribia kumiliki hizo silaha wasijeshangaa mitambo yao inalipuliwa vibaya kwani inavyoonekana ni kwamba intelijensia ya Israel iko karne nyingi mbele ya ile ya Iran.
 
Hii mada imeelezea yale ambayo Mossad imefanikiwa kuyafanya katika Iran. Hoja husika imeungwa mkono na wasemaji kutoka Iran yenyewe na ndani ya Israeli. Kama unataka kuleta habari ya upande wa pili wa hizi habari, kama upo,anzisha mada na tutachangia kadiri tuwezavyo.
Usichojua kwanza, nchi zote za kiarabu walifukuza wayahudi wao, kasoro iran ambao ni majirani na waarabu,
Lakini hata hivyo israel haitumii sana wayahudi walioko iran kuhujumu iran
Bali, ujua serikali ya sasa ya iran ni ya mapinduzi. Sasa waliopinduliwa wapo walioko nje ya iran lakini pia wapo waliomo ndani
So israel inawa Recruit hawa wapinzani, na ndio wanaotoa ramani na kuelekezwa wakafanye nini ndani ya iran,,,
Usidhani eti mossad kama mossad huingia iran kuhujumu na kuchomoka kurudi kwao,,
 
Israel is over rated, nawanatumia propaganda nyingi kwaminisha watu kwamba technology yao ni sophiscated sana, Israel imeshindwa vita nyingi na inapigwa sana isipokua wegi hawalifahamu
Wewe unauefahamu tujuze..kama propaganda na wengine si watumie..kuna aliewakataza kutumia hizo propaganda..shida binadamu kam wewe hua hamtaki kukubali kua kuna wenye uwezo sikuzote binadamu hatuwezi fanana..always there's a big fish than you in the ocean.

#MaendeleoHayanaChama
 
Usichojua kwanza, nchi zote za kiarabu walifukuza wayahudi wao, kasoro iran ambao ni majirani na waarabu,
Lakini hata hivyo israel haitumii sana wayahudi walioko iran kuhujumu iran
Bali, ujua serikali ya sasa ya iran ni ya mapinduzi. Sasa waliopinduliwa wapo walioko nje ya iran lakini pia wapo waliomo ndani
So israel inawa Recruit hawa wapinzani, na ndio wanaotoa ramani na kuelekezwa wakafanye nini ndani ya iran,,,
Usidhani eti mossad kama mossad huingia iran kuhujumu na kuchomoka kurudi kwao,,
Hata Mossad wakitumia hao unawataja bado inaonekana ni kazi ya Mossad, kwani mbinu na technolojia inakuwa imeandaliwa na Mossad.
 
hio ilikuwa zaman kipindi hiki israel ndio imekuwa ikipelelezwa na iran vibaya mno juza kati mfanyakazi wa waziri wa ulinzi wa israel alikatwa kwa tuhuma za kuipa iran taarifa muhimu mpaka iran ikapata password za makampuni makubwa ndani ya israel na marekani
 
Israel is over rated, nawanatumia propaganda nyingi kwaminisha watu kwamba technology yao ni sophiscated sana, Israel imeshindwa vita nyingi na inapigwa sana isipokua wegi hawalifahamu
Sasa wewe unayejua tueleze tuelewe
 
Propaganda tu zisizo na kichwa wala miguu, USA na Mtoto wake Israel wamemshindwa Iran toka Israel ilipoanzishwa mwaka 1948 hadi Leo.
 
Hii mada imeelezea yale ambayo Mossad imefanikiwa kuyafanya katika Iran. Hoja husika imeungwa mkono na wasemaji kutoka Iran yenyewe na ndani ya Israeli. Kama unataka kuleta habari ya upande wa pili wa hizi habari, kama upo,anzisha mada na tutachangia kadiri tuwezavyo.
Umemjibu vizuri sanaa maana hata mimi sikumelewaa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom